HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 2 November 2017

BALOZI MBAROUK AKABIDHI HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA JAMHURI YA KIISLAM YA IRAN

Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, mwenye Makazi yake Umoja wa nchi wa Falme za Kiarabu (U.A.E) akikabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mhe. Rais Hassan Rouhani. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ikulu ya Rais, Mjini Tehran tarehe 28 Oktoba, 2017.
Mhe. Rais Hassan Rouhani akisoma hati za utambulisho alizokabidhiwa na Mhe. Balozi Mbarouk, ambapo alitumia fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Mbarouk na kuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mhe. Rais Hassan Rouhani akizungumza na Mhe. Balozi Mbarouk mara baada ya kukabidhi hati. Katika mazungumzo yao wameahidi kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano kwa lengo la kukuza uchumi wa mataifa yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad