HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 13, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE:WATANZANIA JITOKEZI KUMSHANGILIA BONDIA WETU IBRAHIM CLASS

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia) akitoa wito kwa watanazania  kujitokeza kwa wingi uwanja wa uhuru tarehe 25/11/2017 kushangilia pambano la bondia Ibrahim Class (kushoto)  wanchini akitetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini leo jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo  kambini  Joe Gym  Kawe. yake ya mazoezi.
 Bondia Ibrahim Class (kulia) akifanya mazoezi na Mwalimu Msaidizi Bw.Kelvin Magembe (kushoto) kuonyesha uwezo wake mbele ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia)alipomtembelea kambini Joe Gym  Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano litakalofanyika kati yake na Bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017 Uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
 Bondia Ibrahim Class (kulia) akimkabidhi  zawadi ya tisheti yenye jina lake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) alipomtembelea bondia huyo  kambini Joe Gym  Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano la tarehe 25/11/2017 katika uwanja wa uhuru na bodia wa Afrika ya Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati leo jijini Dar es Salaam.

Na Anitha Jonas WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kumshangilia bondia Ibrahim Class katika pambano lake la kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia kutoka Afrika ya Kusini  Koos  Sibiya.
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa wito huo jana  jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo kambini Joe Gym Kawe kujionea maandalizi yake bondia  kwa pambano litakalofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017.
“Bondia huyo anauwezo mkubwa na amekwisha kushinda mara mbili kwa Afrika na kwa mkanda huu wa kugombea ubingwa wa dunia nimeona ni vyema akapigania hapa nchini ili watanzania waweze kuona uwezo wake na pamoja na kumongezea ari ya kupambana kwa ajili ya watanzania walikuja kumuunga mkono,”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea  kuzungumza katika ziara hiyo Mhe. Mwakyembe alisema  atasimamia mchezo wa ngumi na kuhakikisha unarudisha heshima yake kama ilivyokuwa zamani kwa kuhakikisha anadhibiti wapiganaji wanaokwenda kwenye mapambano na kununuliwa huku wakililetea sifa mbaya taifa ya kutumika kupandisha watu madaraja.
Kwa upande wa Bondia Ibrahim Class wa nchini aliwahakikishia watanzania kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha anauchukua ubingwa huo na mkanda huo kubaki nchini huku akiwataka watanzania kuja kujionea wenyewe namna atakavyopambana na kuonyesha uwezo wake.
“ Nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa  waje kujionea wenyewe jinsi gani nitakavyo mpiga huyo mwafrika kusini na kuchukua mkanda nimejiandaa vizuri na mazoezi ninayofanya niyakiwango cha juu,”alisema bondia Class.
Pamoja na hayo nae Rais wa TPBC Bw.Chaurembo Palasea aliongeza kuwa mchezo wa ngumi umekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ulingo kwa ajili ya kufanyia mazoezi kwani hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu kwa sekta ya mchezo wa ngumi. 
Halikadhalika Waziri Mwakyembe  amesema kuwa serikali itaanzisha bodi itakayosimamia sekta ya ngumi kwa lengo la kuondoa kukosekana kwa dira ya usimamizi wa sekta ya ngumi nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad