HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 12 November 2017

WATU WAWILI WAMEFARIKI KATIKA AJALI WILAYANI IKUNGI

Watu wawili wamekufa papo hapo na wengine wawili wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Ikungi,kufuatia gari aina ya Toyota Landcruiser kugongana uso kwa uso na basi la Taqwa.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Sigida SSP Isaya Mbughi amesema,ajali imetokea katika kijiji cha Kideka wilayani Ikungi  majira ya saa tano asubuhi na imehusisha basi la Taqwa lenye usajili wa nambat 159 CWH lilokuwa likitokea Kampala  nchini Uganda na kuelekea jiji Dar-es-Salaam ,kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Toyota Landcruiser yenye usajili wa namba T 862 DJN ilyokuwa ikitokea Dodoma,na kusema chanzo cha ajali ni uzembe wa gari dogo kuliafuta basi.

Mganga wa zamu wa hospitali ya mkoa wa Singida daktari Ramadhani Irunde amethibitisha kupokea maiti mbili zilizotambulika kwa majina ya Inocent Ngonyani na Gabriel William  ambao wamepata majeraha kichwani na  kuvujia damu ndani ya mwili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad