HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 7 November 2017

WASHINDI WA DROO YA KWANZA WA PROMOSHENI YA ZALI LA MWANASPOTI WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

KAMPUNI ya Mwananchi Communications Limited kupitia Gazeti la Michezo la Mwanaspoti, imekabidhi zawadi za droo ya kwanza ya Promosheni ya Zali la Mwanaspoti ikiwa ni zawadi kwa wasomaji kuelekea mwisho wa mwaka.

Zawadi hizo mbalimbali sita zikiwemo simu mbili(Smartphone), Tv mbili nchi 32 zikiwa na vinga’amuzi vyake vya Azam huku zikiwa zimelipiwa mwzi mzima,Pikipiki moja na ticketi moja ya kwenda kushohudia moja ya mechi kubwa nchini Wingereza.

Makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Mwananchi Communications Limited, Sarah Munema (kushoto) akimkabidhi Mbaraka Shomari, zawadi ya simu ya mkononi(Smartphone) mshindi wa droo ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti katika hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Mwananchi Communications Limited, Sarah Munema (kushoto) akimkabidhi Ibrahim Yohana, zawadi ya TV nchi 32 ikiwa na king’amuzi cha Azam TV kikiwa kimelipiwa mwezi mzima mshindi wa droo ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti katika hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.
Meneja wa vipindi vya Michezo wa Azam TV, Baruani Mhuza(kulia) akimkabidhi Ibrahim Yohana, zawadi ya TV nchi 32 ikiwa na king’amuzi cha Azam TV kikiwa kimelipiwa mwezi mzima mshindi wa droo ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti katika hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Masoko wa Mwananchi Communications Limited, Sarah Munema.
Meneja Masoko wa Mwananchi Communications Limited, Sarah Munema (kushoto) akimkabidhi Mkombozi Mubanga, zawadi ya TV nchi 32 ikiwa na king’amuzi cha Azam TV kikiwa kimelipiwa mwezi mzima mshindi wa droo ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti katika hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.
Meneja wa vipindi vya Michezo wa Azam TV, Baruani Mhuza(kulia) akimkabidhi Mkombozi Mubanga, zawadi ya TV nchi 32 ikiwa na king’amuzi cha Azam TV kikiwa kimelipiwa mwezi mzima mshindi wa droo ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti katika hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Masoko wa Mwananchi Communications Limited, Sarah Munema.
Mshindi wa Pikipiki, Joachim Gibson akikabidhiwa Kadi na Funguo wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa droo ya kwanza ya Promosheni ya Zali la Mwanaspoti iliyofanyika Viwanja vya Taifa.
Meneja Masoko wa Mwananchi Communications Limited, Sarah Munema (kushoto) akimkabidhi Aristides Alphonce, zawadi ya ticketi ya Uingereza mara baada ya kuibuka mshindi wa droo ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti katika hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad