HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 6, 2017

Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Bi. Jenista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi  Mtendaji wa FERUSCO Sustainable Development,Bw. Felisi Ngonyani mbele mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.2 wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo katika mikoa ya kanda ya ziwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Beng’i Issa  wapili kulia, Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi wa tatu kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita na Mbunge, Bw. Joseph Musukuma kulia na Meneja Tawi  TPB Mwanza, Bw. Shaban Telatela kushoto. (Picha na mpiga picha wetu, Geita)
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama  wa tatu kulia akimkabidhi mfano wa hundi Mkurugenzi wa Mtandao wa ViVOBA Endelevu (Visudent) Kamara Mohamed kulia, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa wa pili kulia, Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi wa watu kushoto, Meneja Tawi  TPB Mwanza, Bw. Shaban Telatela kushoto. (Picha na mpiga picha wetu, Geita).
Wanachama wa Vikundi vya VICOBA wakiwa katika uzinduz wa utoaji wa mikopo ya uwezeshaji ambapo vikundi 272 vilipata mikopo toka Benki Posta (TPB) na Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance Chini ya Udhamini wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), (Picha na mpigapicha wetu, Geita).

Na Mwandishi wetu, Geita
Vikundi vya VICOBA 272 vya mikoa ya Kanda ya Ziwa vimenufaika na uwezeshaji wa mikopo ya Tsh. bilioni 2. 8 toka Benki ya Posta (TPB) na Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance PLC ili wanachama wake waweze kuitumia katika shughuli za ujasiriamali na kushiriki katika uchumi wa taifa lao.

Vikundi vya VICOBA vilivyo nufaika na mikopo hii vinatoka katika Wilaya au halmashauri za Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Mara kwa lengo la kuviwezesha viweze kushiriki katika kuondoa umasikini miongoni mwa wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo hiyo mkoani Geita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Bi. Jenista Mhagama alisema mkopo huo ni sehemu ya Uwezeshaji wananchi kupitia vikundi vya ViCOBA ili waanzishe au waimarishe miradi yao ya ujasiriamali.

 ‘’Huu ni uwezeshaji Mkubwa na tunataka mkatumie fedha hizi kuendeleza miradi yenu ya ujasiriamali ili ikazalishe na muweze kuondokana na hali duni ya vipato,” na hiyo pia itawasaidia kushiriki katika uchumi wa nchi,aliongeza kusema,Bi Mhagama.

Mikopo hiyo imetolewa na TPB na UTT Microfinance PLC chini ya udhamini wa Baraza la Taifa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Akifafanua zaidi alisema TPB ilitoa Tsh.bilioni 2.7 kwa vikundi 228 na UTT Microfinance imetoa Tsh.milioni  100, 300,00 kwa vikundi viwili vyenye wanachama 30.

Pia alizitaka taasisi zote za kifedha hapa nchi kuanza kwenda katika wilaya au halmashauri kutoa huduma za kifedha kama mikopo ilia wananchi waweze kuzitumia katika mirdi yaujasiriamali.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Bi. Beng’i Issa alisema mikopo hiyo imedhaminiwa na baraza kupitia mfuko wa taifa wa uwezeshajii wananchi kiuchumi imetolewa kwa masharti nafuu na ni mwendelezo wa udhamini inaoufanywa ili mikopo itolewe kwa wajasiriamali kupitia SACCOS na VICOBA.

“Vikundi hivi ni matunda ya taasisi mwanvuli  zilizokubali kushirikiana na serikali kuvianzisha na kufundisha elimu ya VICOBA,” serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hizi katika kazi ya kuzidi kuwawezesha wananchi aliongeza kusema



Alizitaja taasisi hizo mwamvuliza za VICOBA ni pamoja na Peoples Long Life Initiative (PLI), Ferusco Organisation VICOBA Sustainable Development Agency (FOVSDA), Upepo Wetu na VICOBA Sustainable Development Nertwork VISUDENT.

Kwa Mujibu wa Bi. Issa ni kwamba taasisi hizo mwanvuli pia zitahusika katika kusimamia maresjesho ya mikopo ya vikundi ili kuhakikisha zinarudi kwa wakati na vikundi vingine viweze kupata.

Alisema serikali kwa sasa imejielekeza katika kufikia uchumi wa viwanda na viwanda na  uwezeshaji huo unalenga wananchi wananzishe au kukuza viwanda vidogo vidogo ili mazao ya hapa nchini yaweze kuongezewa tham ani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi alisema mikopo niyo ni ya kujivunia na yenye manufaa makubwa katika kukuza vipato vya wananchi kuondokana na umasikini katika kanda hiyo.

Serikali inafanya kazi kubwa ya kuweka mazingira wezeshi na kuibua fursa na serikali za mikoa ya kanda yetu tutahakikisha mikopo hii inaleta tija,” Wanachama wa vikundi hivyo wanafanya shughuli mbalimbali za kijasiriamali, aliongeza Kusema,Bw. Lughumbi.

Baraza hilo la Taifa linafanya kazi chini ya sheria uwezeshaji namba 16 ya mwaka 2004 na limedhamiria kuhakikisha uwezeshaji huo unawakomboa wananchi kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad