HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 28 November 2017

TIGO KUWAMWAGIA SIMU WATEJA WAKE MSIMU HUU WA SIKUKUU

Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh (kushoto) akifafanua jambo wakati akizungumzia ofa ya kipekee kwa wateja wa Tigo kuhusu simu za Smartphone ambazo zitahakikisha kila mtu anakuwa sehemu ya maisha ya kidigitali katika msimu huu wa Krismasi na mwaka mpya, uliofanyika katika Ukumbu wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Mawasiliano, Woinde Shisael
Meneja Mawasiliano, Woinde Shisael akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati akizungumzia ofa ya kipekee kwa wateja wa Tigo kuhusu simu za Smartphone ambazo zitahakikisha kila mtu anakuwa sehemu ya maisha ya kidigitali katika msimu huu wa Krismasi na mwaka mpya, uliofanyika katika Ukumbu wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania, leo imetangaza dili za kipekee zinazohusu simu za Smartphone ambazo zitahakikisha kila mtu anakuwa sehemu ya maisha ya kidigitali katika msimu huu wa Krismasi na mwaka mpya.

Akitangaza ofa hizo za msimu wa sikukuu Dar es Salaam leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema dili hizo kemkem zinapatikana kwa kupiga namba ya menu mpya *147*00# na kubonyeza kitufe cha ‘Duka la Simu’ ili kuchagua simu unayoipenda, na kisha kutembelea Duka lolote la Tigo nchi nzima ili kuchukua simu uliyoichagua.

‘Katika ofa ya kwanza, wateja wa Tigo wanaweza kupata simu ya Smartphone BURE kirahisi kwa kununua bando kuanzia TZS 25 000 ambayo - pamoja na Smartphone ya bure – inawapa 1GB data, SMS 50 na dakika 50 za kupiga Tigo – Tigo,’ alisema.

Katika dili ya pili, wateja wa Tigo pia wanaweza kupata Smartphone kwa kuchagua mpango wa kulipia kwa miezi sita. Ofa hii inawahusu wateja wa sasa wa Tigo ambao wanakidhi vigezo vilivyowekwa.

Katika msimu huu wa sikukuu, Tigo pia inatoa ofa ya ‘Lipia sasa, Chukua Baadaye’ ambapo wateja wanaruhusiwa kuchagua simu yoyote ile wanayoipenda na kisha kufanya malipo ya awamu kila mwezi, ambapo wataruhusiwa kuchukua simu waliyoichagua baada ya kumaliza mpango wa malipo ya kila mwezi.

‘Kupitia ofa hizi kabambe, Tigo inaendelea kushika hatamu za ubunifu unaoendana na mahitaji ya wateja kwa kuwezesha kila mtu kumiliki mojawapo ya hizi simu bomba za Smartphone, ambazo zimeunganisha na mitandao ya jamii. Hii ndio njia yetu ya kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa sehemu ya maisha na mabadiliko ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo,’ David alisema.

‘Tunawakaribisha wateja wetu wachangamkie ofa hizi za kipekee katika msimu huu wa sikukuu kwa kujigiftisha au kuwagiftisha ndugu, jamaa na marafiki kwa simu hizi bora za smartphone. Simu zote zinakuja na mpango rahisi wa malipo, bando murwa na ofa za kipekee ambazo zitahakikisha kila mtu ataweza kufurahia na kutunza kumbukumbu za shamrashamra za sikukuu katika simu yake mpya ya smartphone kutoka Tigo.’

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad