HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 2, 2017

TFDA YAZIDI KUNGARA KATIKA UDHIBITI DAWA NA VIFAA TIBA KATIKA NCHI ZA AFRIKA –WAZIRI UMMY MWALIMU

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya meza kuu na wageni wa alikwa, tukio lililojiri katika viunga vya Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA).
 Watumishi wa umma na wageni waalikwa wakiwa wakifuatilia kwa ukaribu taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu(MB) hayupo kwenye picha, mapema katika uzinduzi wa Maabara hamishika uliofanyika katika ofisi za TFDA.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara hamishika hizo, wakwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa, watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya TFDA Bi. Zainabu na wa mwisho ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Hiiti B. Sillo.
Mh. Ummy Mwalimu akipata maelekezo kuhusu Maabara hamishika hiyo wakati wa uzinduzi wa maabara hamishika mapema leo katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa.
 Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maabara hamishika mapema katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekuwa ni Taasisi bora kwa Bara la Afrikakatika kudhibiti dawa na chakula ili watanzania wapate huduma bora.
Ummy ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Maabara Hamishika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa katika kulinda afya za  wananchi ni kupata dawa zinazostahili ambazo zimedhibitiwa na TFDA.
Amesema kuwa matumizi ya dawa zisizo sahihi zinarudisha kasi ya uchumi ambayo inatokana na watu kuingia  gharama za kununua dawa hizo mara kwa mara na tatizo kubaki pale pale.
Ummy amesema kuwa licha ya kudhibiti dawa lakini TFDA isiwe kikwazo cha uwekezaji katika sekta ya viwanda ambapo wawekezaji wanatakiwa kufuata taratibu za nchi zilizowekwa.
Aidha amesema kuwa kazi ya TFDA ni kuhakikisha afya za wananchi zinalindwa kwa kuwa na wananchi wenye afya njema na wanaweza kuwfanya kazi na kuliletea Taifa maendeleo.
Amesema TFDA inatakiwa kuzingatia tathimini ya kina ya kisanyasi pamoja na matokeo ya uchunguzi wa maabara hivyo maabara  ya TFDA ni kiungo muhimu katika kutekeleza jukumu la kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa hizo.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema jukumu la TFDA ni kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa wa bidhaa ya chakula na dawa, vipodozi na vifaa tiba na vitandanishi ili kulinda afya ya jamii dhidi ya madhara yanayoweza kutokana na matumizi ya bidhaa duni na bandia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad