HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 27 November 2017

TBL YAJITOSA KATIKA KAMPENI ZA KUPINGA UKATILI WA JINSIA

 Waziri wa Madini, Mh. Angela Kairuki akibadilishana na mawazo na Kaimu Mkurugenzi wa WiLDAF,Anna Kulaya wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiwa na bango lenye ujumbe wa No Excuse wakati wa maandamano ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL na wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya uzinduzi wa kampeni ya No Excuse. ---

Kampuni ya Tanzania Breweries Limited na kampuni zake tatu (TBL Group) chini ya kampuni mama ya AB INBEV mwaka huu imeungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hasa watoto wa kike.

Maadhimisho haya ambayo yalizinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Waziri wa Madini,Mh,Angela Kairuki, huandaliwa kila mwaka na Shirika lisilo la kiserikali la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika- (Women in Law and Development in Africa -WiLDAF) kwa kushirikiana na mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia nchini (MKUKI),wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali za kiserikali na za binafsi.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya mwaka huu ni ‘Funguka!ukatili dhidi ya wanawake na watoto haumuachi mtu salama.Chukua hatua ‘ ambayo inalenga kuhimiza kuelimisha jamii ya watanzania kubadilika na kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikitokea kwenye jamii.

Afisa Mawasiliano wa TBL,Amanda Walter, amesema katika mahojiano maalumu kuwa TBL itatumia njia mbalimbali kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ikiwemo jumbe kupitia redio,magazeti na mitandao ya kijamii. Vile vile wafanyakazi wa kampuni ya TBL wameungana na jamii katika kushiriki katika maandamano ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki .

“TBL imeamua kutumia maadhimisho hayo kupeleka ujumbe kwa jamii kuacha kujihusisha na matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia kupitia kampeni inayojulikana kama “Acha Sababu,badilika” -(#NoExcuse)”Alisema Walter.

Alisema TBL imeshiriki kampeni hii ya kuhamasisha mabadiliko dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa sababu, , TBL ni kampuni inayoongoza nchini hivyo basi kati ya majukumu lake katika jamii moja yapo ni swala zima la unywaji pombe kiistarabu na pia kwamba pombe isewe na isitumike kama sababu ya ukatili wa kijinsia,TBL ina sera ya uhamasishaji utumiaji wa vinywaji vyenye ulevi kistaarabu kwenye jamii ili kuepusha madhara mbalimbali yatokanayo na matumizi yenye vinywaji vyenye kilevi kupita kiasi .

Walter aliongeza kusema kuwa kampeni hii ya -#NoExcuse itaenda sambamba na kutoa jumbe mbalimbali za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii sambamba na matukio mengine yanayotokea na kuhusisha na ulevi kama vile kufanya uzembe wakati wa uendeshaji wa vyombo vya moto na kusababisha ajali.

“Jumbe za kampeni hii yetu ya #NoExcuse zitahamasisha jamii kubadilika na kuacha vitendo mbalimbali vinavyoleta athari kwenye jamii kama vile vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake,vitendo vya ukatili dhidi ya wanaume,vitendo vya kupigana,vitendo vya ubakaji,utumiaji wa lugha za matusi zenye kudhalilisha watu wengine,uasherati n.k”.Alisema.

TBL inaamini kuwa ukatili wa kijinsia unaweza kutokomezwa nchini endapo jamii nzima itashirikiana na kukemea vitendo hivyo kwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha vyombo vya maamuzi vinavalia njuga suala hili na itaendelea kuunga mkono kampeni hizi siku zote.

Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa WiLDAF,Anna Kulaya kwa niaba ya asasi za kiraia zinazoshriki katika kampeni hii aliiomba serikali kutunga sheria za ukatili wa majumbani (Domestic Violence Act),Kuanzisha mahakama za familia ili kuharakisha kesi na hivyo kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati,kuharakisha mapitio ya sheria kandamizi zote zinazowabagua wanawake na watoto na kuboresha miundo mbinu rafiki hasa kuwa na maeneo ya kuhifadhi wahanga wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad