HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 8 November 2017

TANZANIA NA SWEDEN YAADHIMISHA MIAKA 40 YA USHIRIKIANO WA MASUALA YA UTAFITI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano wa masuala ya utafiti baina ya Tanzania na Sweden na namna walivyoweza kufanikiwa kupata wataalamu mbalimbali wa tafiti. 


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amesema kuwa ushirikiano uliopo baina ya  nchi ya Tanzania na  Sweden umeweza kuleta tafiti zenye tija kwa taifa na kufanikisha kupatikana kwa watafiti mbaimbali.

Hayo  ameyasema leo katika maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano wa masuala ya utafiti baina ya Tanzania na Sweden yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya utafiti nchini.

Dkt Akwilapo amesema kuwa, ushirikiano huo umeweza kuwasaidia katika kufanya tafiti zenye tija na maamuzi yanayoendana na tafiti kwa njia bora, wameweza kunufaika kwa kuweza kupata watafiti mbalimbali ambao wengi wao walikuwa wanafunzi.
"Kwa kipindi cha miaka 40 ya ushirikiano wetu baina ya Tanzania na Sweden tumeweza kupata watafiti wengi sana ambao kwa sasa wameweza kuhitimu katika ngaza za uzamivu (PHD) kwenye masuala mbalimbali ambapo wamweza kupatikana na kufanya tafiti mbalimbali kipindi wanasoma,"amesema Dkt Akwilapo.

Kwa upande wa  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dugushilu Mafunda amesema amesema kuwa baada ya kuwezeshwa kwa kipindi ca miaka 10 wameweza kupata watafiti ambao kwa sasa hivi wanawafundisha watu wengine namna ya kufanya tafiti pia tafiti hizo zimejikita zaidi katika sayansi na teknolojia.

Mafunda ameongeza lengo kubwa ni kuhakikisha taasisi zijiendeshe, kuweza kuzipa taasisi nguvy ya kwenda kufanya tafiti sehemu mbalimbali na wanashukuru kwa sasa serikali ya Tanzania wanatilia mkazo suala la sayansi na teknolojia.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya utafiti ya nchini Sweden,  SIDA nchini Sweden Karin Jamtinameweka wazi kuwa kwa sasa Tanzania wameweza kukua katika masuala ya utafiti na zaidi wameshapata wataalamu kutoka kwa wanafunzi waliokuwa wanafanya utafiti kwenye miaka ya nyuma na hilo limeweza kusaidia zaidi kwenye kutoa elimu.

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dugushilu Mafunda akielezea namna ushirikoano huo baina ya Tanzania na Sweden ulivyoweza kusaidia kuwapata wataalamu na utafiti pia kuweza kuwasadia taasisi kujindesha zenyewe ikiwemo kufanya tafiti sehemu tofauti za nchi na nje ya nchi.
Makamu wa Rais Mstaafu Gharib Bilal (kulia) akifuatilia mkutano wa maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano wa masuala ya utafiti baina ya Tanzania na Sweden ulioanza leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya utafiti ya nchini Sweden, SIDA nchini Sweden Karin Jamtin akizungumza na wanahabaru namna jinsi taasisi yao ya nchini Sweden walivyoweza kushirikiana na Tanzania kupitia vyuo na serikali kwenye masuala ya utafiti wa mambo mbalimbali.
Wadau wa masuala ya sayansi na teknolojia wakiwa wanatembelea mabanda yaliyopo katika ukumbi wa mkutano ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano wa masuala ya utafiti baina ya Tanzania na Sweden yalioanza leo Jijini Dar es Salaam


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad