HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 7 November 2017

TAMBWE, KAMOSOKU NA NGOMA MATARAJIO NI KUANZA MAZOEZI MEPESI WIKI HII- DR BAVU

Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tz Prison Novemba 19.

Mazoezi hayo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru, Yanga  wamefanya mazoezi bila nyota wao nane walioitwa katika timu za taifa pamoja na mjeruhi watatu ambao ni kiungo Thabani Kamusoko, Washambuliaji Donald Ngoma  na Amissi Tambwe.

Lakini imewakosa wachezaji wake watano walioitwa katika timu za taifa kubwa na ile ya vijana.
Walioitwa katika timu ya taifa, Taifa Stars ni Ramadhani Kabwili, Kelvin Yondani, Gadiel Michael, Raphael Daud na Ibrahim Ajibu Migomba.

Kwa mujibu w daktari wa timu Dr Edward Bavu  ameweka wazi kuwa majerehui hao wanaweza kurejea dimabni Novemba 10 kwa ajili ya kuanza mazoezi mepesi na kisha kujiunga na wenzao kwa mazoezi ya pamoja.

Kwa sasa hawajafika asilimia 100 ila sio Ngoma pekee, bali hata kiungo  Kamusoko na Tambwe pia wanaweza kuanza mazoezi wiki. Matarajio yetu hadi wiki ijayo watakuwa wameungana na wenzao kikamilifu."

Ngoma ambaye kwa sasa yupo nchini kwao akiendelea na matibabu atarejea siku yoyote kwa ajii kujiunga na wenzake akianza mazoezi ya taratibu.

Yanga wanaoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 17 wataumana na Tz Prisons wakiwa wametoka kupata sare tasa dhidi ya Singida United mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad