HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 14, 2017

TAIFA STARS YAREJEA DAR, KUSUBIRI MAANDALIZI YA CHALLENJI

Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imereja alfajiri ya leo salama kutoka nchini Benin walipokuwa wameenda kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin.

Stars iliyokuwa ugenini iliweza kutoka sare kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji Benin uliofanyika Uwanja wa La Amitie jijini Continou na kutoka sare ya 1-1.

Mara baada ya kurejea, kambi ya Stars ilivunjwa kwa wachezaji kusafirishwa kwenda kwenye timu zao kadiri ya makubaliano kuanza maandalizi ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom, Tanzania Bara inayoendelea mwishoni mwa wiki.

Safari hii Stars imecheza mechi yake bila nyota wake wanne wakiwamo Erasto Nyoni na Muzamiru Yassin ambao walikuwa wanatumikia kadi nyekundu huku Nahodha wa timu, Mbwana Samatta na Kiungo mahiri, Farid Mussa ambao ni majeruhi.

Taarifa kutoka Genk ya Ubelgiji, zinasema kwamba Mbwana Samatta amefanyiwa upasuaji mdogo katika goti la kulia na mpaka kupona, itamchukua hadi wiki nane ili kurejea uwanjani.

Wachezaji waliorejea ni Aishi Manula, Peter Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Himid Mao, Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Faridi Mussa, Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na Elias Maguli.

Wakati huo huo, kambi ya timu ya Taifa ya Vijana Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro Warriors’ inatarajiwa kufikia ukomo Alhamis Novemba 16, mwaka huu.

Timu hiyo yenye wachezaji 34 kutoka timu mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzana Bara, ipo kambini kwa ajili ya mchujo wa kupata wachezaji wasiozidi 25 watakaunda kikosi kamili cha vijana wenye umri wa chini ya miaka 23.

Kadhalika, Serengeti Boys – Timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, wanatarajia kuingia mwishoni mwa mwezi huu kujiandaa na michuano ya kuwania Kombe la Chalenji kwa vijana itakayofanyika Burundi kuanzia Desemba 12 hadi 22, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad