HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 17 November 2017

TaESA YAPITIA UTEKELEZAJI WA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANACHUO 100, SITA WAONDOLEWA KWA UTOVU WA NIDHAMIU

 Mkurugenzi Mtendaji wa  Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania  (TaESA) Boniface Chandaruba akizungumza na baadhi ya wanachuo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya wanachuo 100 walioteuliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa kushirkiana na Wakala wa Serikali  waliokatika mradi wa awali kwa wanachuo wa mwaka wa kwanza  kupata mafunzo kutoka kwa mashirika na taasisi mbalimbali ikiwa ni katika kipindi cha miaka 3.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) imewataka wanachuo waliopata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo kutilia mkazo suala hilo utovu wa nidhamu unaweza kuwakosesha na kuondolewa kwenye mchakato huo ambapo tayari wanafunzi sita wameondolewa.

Akizungumza na baadhi ya wanafunzi hao katika mkutano wa majadiliano ya tathmini ya utekelezaji
wa mafunzo kwa vitendo kwa wanachuo 100 wa mwaka wa kwanza  kutoka Chuo Kikuu ca Dar es Salaam kwa awamu ya kwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa TaESA Boniface Chandaruba amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kutilia mkazo suala hili kwani wameweza kupata nafasi ya kipekee kwa kuwezeshwa kufanya mafunzo ya vitendo ikiwa bado hawajamaliza chuo.

Chandaruba amesema kuwa, ILO imeweza kuleta mradi huo kwa lengo la kuwaandaa wanachuo pindi wanapomaliza chuo wanakuwa tayari wameshapata uzoefu pia hata zile taasisi wanazofanyia kazi wanauwezo wa kuwapa ajira.
Mradi huu unaodhaminiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) umelenga hasa katika kuwasaidia wanafunzi hususani wana vyuo kupata uzoefu utakaowasaidia baadae katika kupata ajira ikiwemo kufahamu mazingira tofauti ya kazi pale wanapofanyia lwa kipindi cha mafunzo kwa vitendo.

 Kwa upande Mshauri  wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Paulina Mabuga amesema kuwa mradii ni mzuri pia unaweza kuwasaidia wanavyuo kupata uzoefu katika maeneo wanayofanyia kazi na mategemeo yao makuu ni idadi inaongezeka katika awamu ya pili ya wanafunzi watakaochaguliwa kwa ajili ya mafunzo hayo kwa vitendo.

Moja ya waajiri kutoka Baraza la Sanaa la Taifa ( BASATA) Kitengo cha Fedha na utawala Onesmo Kayanda amewataka wanafunzi wanaopata nafasi kama hiyo kujituma zaidi na kujitolea kwani unapokuwa unafanya vizuri unakuwa unajenga uzoefu mzuri na hata waajiri wanaweza kupendezewa na juhudi zao na hatimaye kukuajiri kabisa.

Wanafunzi hao wameonekana kupendezwa zaidi na hatua hii ya TaESA na ILO kwa kupewa nafasi hiyo ya kupata mafunzo kwa vitendo na pia chuo chao kikiwa cha kwanza kwenye mradi. 
Mshauri wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Paulina Mabuga akizungumzia mradi wa utekelezaji wa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi 100 unaoratibiwa na Wakala wa Huduma kwa Ajira Tanzania (TaESA) wakishirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO).Moja ya waajiri kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kitengo cha fedha na utawala Onesmo Kayanda akizungumza namna walivyoweza kushirikiana na wanachuo hao katika mradi huo na kama angepewa nafasi ya kuwaajiri basi angetoa ajira kwa wanachuo watatu ambao wamefanya vizuri sana kwa kipindi cha miaka mitatu.
Moja ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Takwimu akizungumzia mardi huo na jinzi gani umeweza kumsaidia kwa kuweza kukutana na watu mbalimbali pia uzoefu alioupata kupitia mafunzo kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad