HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 27, 2017

RC WANGABO AITAKA MANISPAA YA SUMBAWANGA KUBORESHA MASOKO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameitaka Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha wanaboresha mazingira ya masoko yaliyopo kwenye Manispaa hiyo ili wananchi waweze kupata huduma kwenye maeneo hayo bila ya kulazimika kufika katikati ya mji kupata huduma hiyo.

Amesema kuwa wakuu wa idara katika Manispaa hawanabudi kuhakikisha wanashuka kuwafuata wananchi na wafanyabiashara wa masoko hayo na kusikiliza kero zao na kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya masoko hayo ikiwemo majengo, usafi wa mazingira na vyoo.

“Nimeambiwa changamoto nyingi sana na wafanyabiashara wa soko la sabasaba na wamekuwa wakifanya biashara zao kwenye mazingira machafu hali ambayo haizoeleki na haifai kuendelea kuwepo, hivyo manispaa lazima iweke kambi kusikiliza kero zao na kuzitatua, kwani lipo kwenye uwezo wao,” Mh. Wangabo alisisitiza.

Aidha, ameitaka manispaa hiyo kuhakikisha usalama wa biashara za wafanyabiashara hao unaimarika ili kupunguza malalamiko yao na kuongeza kuwa atahakikisha malalamiko hayo yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

Akielezea changamoto za soko la sabasaba, Mwenyekiti wa soko hilo Feston Mwilema amesema kuwa changamoto kubwa ya soko hilo ni usalama na kuwa hakuna kituo cha polisi na wala hawana mgambo wa kulinda soko hilo, na kuomba kusafisihiwa mazingira kutokana na uchache wa vifaa vya kuzolea uchafu unaozalishwa katika soko hilo.

“Tumelazimika kuchimba shimo la muda la kutupia uchafu unaozalishwa na wauza samaki kutoka na kutokuwepo kwa shimo la kisasa, na tuna kontena moja badala ya matatu ambalo huzidiwa na soko kukosa uzio ni jambo linalotoa mwanya kwa vibaka kuendelea na wizi,” Alisema Mwilema.

Mh. Wangabo alitembelea masoko nane yaliyopo kwenye manispaa ya Sumbawanga na kubaini kuwa masoko mengi hayatumiki kwa kukosa miundombinu bora na usimamizi na hatimae wananchi kuanzisha masoko yasiyorasmi na kuhatarisha usalama wa bidhaa zao na usalama wa vyakula kutokana na kuvidandaza chini na kuhatarisha usalama wa wanunuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Matola katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu toka kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa samaki wa soko la Sabasaba katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa soko la OTC Kizwite katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akinunua bidhaa alipotembelea Soko la Soweto, kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipotembelea Soko la Soweto, kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad