HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 25 November 2017

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA HOSPITALI YA TAALUMA NA TIBA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI KAMPASI YA MLOGANZILA

Na Jonas Kamaleki - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara kuweza katika viwanda vya madawa ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa bidhaa hiyo nchini.
Rais Magufuli ameto wito huo leo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wakati akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Syansi Shirikishi Muhimbili.
“Wafanyabiashara tumieni fursa hii ili muweze kuwekeza katika viwanda vya madawa kwani Tanzania imepewa nafasi ya kuuza dawa katika nchi za SADC na tumetenga zaidi ya bilioni miambili kwa ajili ya kununulia madawa,”amesema Rais Magufuli.
Ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kujenga kiwanda cha madawa Mloganzila badala ya kukkopesha fedha hizo kwa watu wanaojenga nmajumba.
Magufuli amesema kuwa Serikali imedhamira kuwekeza katika masuala ya Afya ili kuwa na Taifa lenye watu wenye afya ili wawezekushiriki katika ujenzi wa viwanda. Bila afya njema hakuna ambacho kitafanyika, alisisitiza Rais Magufuli.
Katika Chuo kitakachojengwa Mloganzila kikitumika apmoja na hospitali hiyo, Rais Magufuli amesema kitatola wataalaam wenye ubora ambao utaendana na hadhi ya chuo hicho.
Ili kuongeza ufanisi katika hospitali za mikoa, Rais ameshauri zisimamiwe na wizara ya afya kuliko ilivyo sasa ambapo zilikuwa zikisimamiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
“Hospitali hizo haziwezikusimamiwa na watu ambao sio wataalaamu wa tiba, hivyo hospitali zote za mikoa ziwe chini ya wizara ya Afya ambayo ndiyo inasimamia Sera ya Afya, na hizo nyingine za wilaya, kata na vijiji ndizo zisimamiwe na TAMISEMI, alisema Rais Magufuli.
Amesema kwa usimamizi huo sekta ya Afya itaimarika kuanzia ngazi ya mikoa hadi Taifa.
Rais Magufuli amewataka madaktari na wahudu wa afya hapo katika Hospitali ya Mloganzila kutunza vifaa na miundombinu ya hospitali hiyo ili kuhakikisha ubora uliopo sasa hivi uweze kudumu.
Amewataka kutoharibu vifaa hivyo vya kisasa ambavyo Rais amesema kuwa Hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa na ina hadhi kama hospitali za Ulaya.
Kwa upande wa Bima za Afya, Rais magufuli amewataka wananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya ambayo itawahakikishia upatikanaji wa matibabu.
“Msiendekeze ununuzi wa nguo, starehe bali changieni katika mifuko hiyo ambayo itawasaidia watoto wenu kupata matibabu ya uhakika, ukiuza majogoo wawili utaweza kumlipia mwanao gharama za matibabu kwa mwaka,”alisisitiza Rais Magufuli.
Aidha, Rais amewataka mawaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kushirikiana katika kuendesha hospitali za Muhimbili na Mloganzila.
Amewambia kuwa umimi hauhitajiki katika masuala ya kitaifa hivyo wizara hizo zishirikiane katika kuhakikisha ufanisi wa Hospitali ya Mloganzila.
Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya ya Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Apolinary Kamuhabwa amesema kuwa Hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa ambavyo vitatumika katika kutoa huduma za tiba ya dhararula kwa watu wazima na watoto, huduma za magonjwa ya akina mama na mfumo wa uzazi, magonjwa ya macho, mfumo wa pua, koo na masikio na magonjwa ya akili.
Kwa mujibu wa Prof. Kamuhabwa huduma nyingine zitakazotolewa na hospitali hiyo ni pamoja na hmatibabu ya magonjwa ya mifupa na majeruhi, upasuaji mkubwa na mdogo, huduma za kusafisha damu kwa magonjwa ya figo na tiba za magonjwa mbalimbali zikiwemo za kinywa.

Hospitali ya Mloganzila imejengwa na Serikali ya Tanzania na Korea ya Kusini ambayo imetoa mkopo wa masharti nafuu. Ujenzi wa Hospitali umegharimu jumla ya Dola za Kimarekani milioni 94.5 (USD) ambapo Serikali ya Tanzania imetoa jumla ya dola za Kimarekani milioni 18.4.               
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole OCS wa Kibamba Mrakibu wa Polisi (SSP)  Pius  Lutumo akipata matibabu wakati akitembelea  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017Msanii Mrisho Mpoto na bendi yake ya Mjomba wakitumbuiza  kwenye sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Wadau wa sekta ya afya na wananchi wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017

Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong akisoma hotuba yake kwa Kiswahili fasaha wakati wa ufunguzi wa  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017. Hospitali hiyo imejengwa na kampuni kutoka Korea Kusini

Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong akipongezwa  na Rais Dkt John Pombe Magufuli baada ya kuhutubia kwa Kiswahili wakati wa ufunguzi wa  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017. Hospitali hiyo imejengwa na kampuni kutoka Korea Kusini
Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong akishukuru baada ya kupongezwa kwa kuhutubia kwa Kiswahili wakati wa ufunguzi wa  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017. Hospitali hiyo imejengwa na kampuni kutoka Korea Kusini
Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong akipongezwa  na Rais Dkt John Pombe Magufuli baada ya kuhutubia kwa Kiswahili wakati wa ufunguzi wa  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017. Hospitali hiyo imejengwa na kampuni kutoka Korea Kusini
Rais Dkt John Pombe Magufuli  akiteta jambo na Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong  wakati wa ufunguzi wa  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017. Hospitali hiyo imejengwa na kampuni kutoka Korea Kusini
Mabalozi wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na mmoja wa wageni kwenye sherehe hizo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameongozana na Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong wakifuatiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia suluhu Hassan, makamu wa Rais Mstaafu Mstaafu Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba wakielekea sehemu ya ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akifunua kitambaa kuashiria kufungua rasmi Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akisaidiwa na viongozi wengine na wadau wa afya akikata  utepe kuashiria kufungua rasmi  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017

Picha za Pamoja na wadau baada ya ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi baada katika sherehe za  ufunguzi wa Hospitali ya

Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga wananchi baada ya sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais Magufuli akisalimiana na wasanii wa bendi ya Mjomba waliotumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga wananchi baada ya sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza mtangazaji wa TBC kwa kazi nzuri ya kurusha mubashara sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo Novemba 25, 2017
 Muonekano wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila baada ya sherehe za ufunguzi leo Novemba 25, 2017

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad