HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 1 November 2017

PPF KANDA YA MASHARIKI WATOA ELIMU YA MWONGOZO WA MAFAO KWA VIONGOZI NA WASIMAMIZI WA SEHEMU ZA KAZI KUTOKA TAASISI BINAFSI, AFYA NA ZA ULINZI

Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Mashariki inayojumisha mkoa wa Morogoro na Tanga ,Joseph Fungo ( kulia) akimkabidhi cheti Mussa Msongamwanja ( kushoto) wa Kampuni ya Ulinzi ya SAKI baada ya kushiriki mafunzo yaliyoandaliwa na Mfuko huo Oktoba 30, 2017 kwa viongozi na wasimamizi sehemu za kazi wa Taasisi binafsi za Afya , na za Ulinzi zilizopo Manispaa ya Morogoro. 
 
Na John Nditi, Morogoro

MFUKO wa Pensheni wa PPF umedhamiria  kuwafikia na kuandikisha wanachama kutoka sekta rasmi na isiyo rasmi wakiwemo vijana ili baada ya kustaafu wabaki katika maisha mazuri  ya uzeeni.

Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda  ya Mashariki inayojumisha mkoa wa Morogoro na Tanga ,Joseph Fungo  alisema hayo Oktoba 30, 2017  wakati akitoa mafunzo na elimu kuhusu Mwongozo wa mafao ya mfuko huo kwa baadhi ya wasimamizi wa kazi kwa niaba ya waajiri katika taasisi  binafsi zinazotoa huduma ya Afya , pamoja na za Ulinzi zilizopo Manispaa ya Morogoro. 

Alisema  ,watanzania wengi wanauelea mdogo kuhusu  sheria ya Mfuko wa hifadhi ya jamii , hivyo ni jukumu la Mfuko wa PPF  kuendelea kutoa  elimu   iwafikie kundi kubwa  waweze uelewa sheria hiyo na hatimaye wajiunge na  Mfuko wa PPF kunifaika na mafao mbalimbali yaoyoewayo kwa faida yao. Hivyo aliwataka vijana waliopo katika  ajira rasmi na zisizo rasmi kuwekeza fedha zao kwenye mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Pensheni wa PPF  ili  baada ya kustaafu  waweze  kunufaika na mafao yao yatakayowaweka wabakie katika maisha mazuri  ya uzeeni.

Fungo  alitaja baadhi ya mafao  hayo , ni la uzeeni , mafao ya elimu ,  wategemezi , ugonjwa , uzazi , kifo na mafao ya kiinua mgongo  na sifahitajika  kwa ajili ya kuweza kunufaika na mafao hayo. Kuhusu Mfumo  wa Wote Scheme  alisema , umelenga kwa wananchi wasio kwenye sekta rasmi wakiwemo wajasiriamali kwa kutoa  fursa ya kujiunga na mfuko  huo.

 Alisema , wanachama wa kundi hilo watanufaika  na  mafao mbalimbali ikiwemo huduma za matibabu, mikopo ya elimu, maendeleo na mafao ya uzeeni. Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda  ya Mashariki alisema, kila mwanachama atapaswa kuchangia kiasi kisichopungua Sh 20,000 kwa mwezi na kuwasilisha michango kadri awezavyo kwa kutegemeana na makubaliano.


Nao washiriki hao  waliupongeza uongozi wa PPF Kanda hiyo kwa kuona umuhimu wa kutoa  elimu kwao ambayo imewapa uelewa mpana kuhusu faida ya mwajiri na mfanyakazi pindi anapojiunga  kwenye  mfuko wa Pensheni kwa ajili ya manufaa  yao wakati wa   uzeeni.
Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Mashariki inayojumisha mkoa wa Morogoro na Tanga ,Joseph Fungo ( kulia) akimkabidhi cheti Sista Edna Mpilimba ( kushoto).ambaye ni msimamzi wa Shule za Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro baada ya kushiriki mafunzo yaliyoandaliwa na Mfuko huo oktoba 30, 2017 kwa viongozi na wasimamizi sehemu za kazi wa Taasisi binafsi za Afya , na za Ulinzi zilizopo Manispaa ya Morogoro.
Baadhi ya viongozi na wasimamizi sehemu za kazi kutoka Taasisi binafsi za Afya ,na za Ulinzi zilizopo Manispaa ya Morogoro wakisikiliza kwa makini Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Mashariki inayojumuisha mkoa wa Morogoro na Tanga , Joseph Fungo Oktoba 30, 2017 alipokuwa wakitoa mafunzo ya elimu ya Mwongozo wa mafao ili kuwawezesha wafanyakazi kujiunga na mafao yanayotolewa na Mfuko huo. 
Baadhi ya viongozi na wasimamizi sehemu za kazi kutoka Taasisi binafsi za Afya , na za Ulinzi zilizopo Manispaa ya Morogoro wakiwa pamoja na Uongozi wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya Mashariki inayojumuisha mkoa wa Morogoro na Tanga ,Oktoba 30, 2017 baada ya kumalizika kupatiwa mafunzo na elimu ya Mwongozo wa mafao ili kuwawezesha wafanyakazi wao kujiunga na mafao yanayotolewa na Mfuko huo.( Picha zote na John Nditi, Globu ya Jamii - Morogoro).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad