HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 16, 2017

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO AWASAA WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI ABIRIA KUACHANA NA MTAZAMO WA MGOMO

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditie amewataka wamiliki  na wadau wa vyombo vya usafirishaji wa abiria hapa nchini kuacha azma yao ya kufanya mgomo ifikapo Desemba Mosi, mwaka huu na badala yake wampe nafasi ili aweze kushughulikia malalamiko yao.

Naibu Waziri huyo alitoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam jana wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa dharula wa wanachama wa Taboa na vyama vingine kama Uwamadar, Darcoboa, Tati na Tatoa ambao ulikuwa ukijadili kanuni za usafirishaji hapa nchini zilizotolewa na SUMATRA.

Nditie aliwataka wamiliki hao kumpa muda ili aweze kuzipitia kanuni hizo na kuona kama zinamapungufu ili aweze kuwalisiliana na Sumatra waangalie namna ya kurekebisha kwa kuwa kanuni zinaweza kurekebishwa.

Aidha alikiri kuwepo kwa penati nyingi kwenye kanuni hizo na kwamba kutokana na kanuni hizo hakuna mmiliki ambaye anaweza kubaki salama iwapo kanuni hizo zitaanza kutekelezwa.

“Nimepitia tu  kwa haraka kanuni hizo na nimegundua kuna panati 57ambazo hata iweje mmiliki yoyote hapa nchini hawezi kuzikwepa ni lazima tu atakumbana nazo endapo kanuni hizo zitaanza kutekelezwa,”amesema.

Amesema serikali haina lengo la kuwakomoa wadau wa usafirishaji kwa kuwa wao wamekuwa wakiingiza fedha nyingi sana na hivyo ipo haja ya kushirikiana nao ili nao waweze kupata faida.

Wakizungumza katika mkutano huo, wamiliki hao walisema kuwa iwapo sheria hiyo itaanza kutumika usafirishaji utakuwa mgumu na kwamba wamiliki hao hawana mgogoro na serikali lakini kutokana na suala hilo hawataweza kutoa huduma hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya usafirishaji ya Ibraline, Ibrahimu Shayo amesema kuwa wamiliki wote walikubaliana kwamba sheria na kanuni hizo zikianza kutumika basi watapaki magari yao majumbani na ni bora magari hayo wayafugie kuku.

Amesema kuwa asilimia 95 ya biashara ya usafirishaji hawatoi fedha mifukoni mwao, isipokuwa wamekuwa wakipata mikopo toka kwenye taasisi za fedha ambazo zimekuwa zikitoza riba kubwa na huku kanuni pia zikiwabana.

Nae,  Mjumbe wa Taboa kutoka mkoni Mwanza, Anuary Said alisema kuwa SUMATRA ni wasaliti sana na wamekuwa wakiwadhalau sana wadau wa usafirishaji kwa muda mrefu sana na haoni kama kuna umuhimu wa kuwepo kwa chombo  hicho.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Atashasta Nditie akizungumza na vyama vya wamiliki wa vyombo vya abiria  jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad