HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 November 2017

Naibu Waziri Ulega akutana na wananchi wa kijiji cha Sunguvuni


 Naibu wa Waziri na Uvuvi,Abdallah Ulega akipokea taarifa ya ujenzi wa Zahanati ya Sunguvuni mkoani Pwani.


Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega  amesema miundombinu ya barabara za vijiji zikijengwa zitafanya vijiji kuinuka kiuchumi.

Ulega aliyasema hayo wakati alipokutana na wananchi wa kijiji cha Singuvuni kata Mkuranga  wilayani Mkuranga, amesema kuwa taasisi ya barabara za vijijini na Mijini Tarura ni suluhisho kwa barabara za vijijini.

Amesema kuwa wananchi wa sunguvuni wanachangamoto ya barabara ambapo changamoto hiyo itatuliwa na Tarura.

Amesema kuwa Tarura itashighulika na  barabara katika wilaya ya Mkuranga na hatimaye wananchi wataweza kuinuka kiuchumi kutokana na miundombinu hiyo.

Katika ziara hiyo ametoa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Sunguvuni pamoja na kuahidi mifuko 20 ya Saruji ili ujenzi huo uende kwa kasi

Aidha amesema kuwa wanachi Sunguvuni wafanye kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo kutokana na kuwa na ardhi yenye Rutuba.

Meneja wa Tarura wilaya ya Mkuranga,Peter Shirima amesema wameshatenga milioni 18 kwa ajili ya kushughulikia sehemu korofi na amesema barabara zote wameshazipitia na kilichobaki ni utekelezaji.
 Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo ,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Sunguvuni mkoani Pwani.
 .Meneja wa Tarura,Peter Shirima akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa barabara.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga, Ally Msikamo akizungumza juu ilani ya CCM na wananchi wa Sunguvuni mkoani Pwani.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
 Wananchi wa unguvuni mkoani Pwani  wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega
Muonekano wa jengo la  Zahanati ya Sunguvuni mkoani Pwani.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad