HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 4 November 2017

MKAZI MMOJA WILAYANI MBOZI AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA MAUAJI

Omary Katesi mkazi wa kijiji cha Sambewe wilaya ya Mbozi mkoani Songwe amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya mahakama kuu kanda ya Mbeya kumkuta na hatia ya mauaji ya kukusudia dhidi ya kaka yake sikujua katesi  kutokana na mgogoro wa kugombania mali za urithi.
Jaji wa mahakama kuu kanda ya mbeya atughanile ngwala ametoa hukumu hiyo wakati wa kikao chenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji mkoani songwe ambapo katika shauri hilo la jinai namba  56/2014  lilikuwa likiwakabili washtakiwa watatu mshitakiwa namba moja maria senye ambaye ni mama wa mshitakiwa namba tatu omari katesi na mshtakiwa namba mbili alikuwa charles lason nzowa.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa washitakiwa kwa pamoja walitenda  la kuua kwa kukusudia kinyume kifungu namba  196/197 cha kanuni ya adhabu tukio ambalo lilitendwa mnamo septemba 23 mwaka 2012  huko sambwewe, ambapo mshtakiwa alikodisha wauaji kisha kumuua kaka yake usiku akiwa amelala na kumjeruhi mke wa kaka yakekwa mapanga ambapo baada ya kunusirika aliwataja wahusika wote akiwemo mama mzazi.
Historia ya tukio imeeleza chanzo cha mauaji hayo ni  ugomvi wa mali za urithi ambazo ziliachwa na baba yao mzazi kates william shega, ambapo sikujua alimshauri kutouza holela mali ambayo ni mashamba na mifugo na kurudisha fedha kwa mmoja  wa wanunuzi wa shamba kwa lengo la kuokoa mali jambo ambalo lilimkera omari na kukodi wauaji kutoka kwa mshitakiwa namba 2 charles lason nzowa kwa shilingi laki 9 na aliyetekeleza  mauaji hayo mshtakiwa huyo namba 2 alifariki akiwa gerezani.
Jaji ngwala amesema kwa maelezo ya mashahidi nane yaliyotolewa mahakamani hapo, pasipo shaka yoyote mahakama imeridhishwa na ushahidi huo na kwamba adhabu ya mtu anayepatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia na ukiri uliotolewa na mshitakiwa mara baada ya kurejea kijijini, kwa kifungu namba 322 sheria ya kanuni ya uendeshaji wa kesi za jinai sura namba 20  iliyofanyiwa marekeshi mwaka 2002, ikamtia hatia nakutoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa.
Aidha jaji ngwala amelazimika kuahirisha vikao vya kusikiliza kesi za mauaji kwa muda usio julikana baada ya mawakili watatu kuugua ghafla wakidaiwa kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu kilichopikwa kwenye mgahawa wa ujulikanao kama be free hotel uliopo vwawa mjini, ambapo mawakili wote wamekimbizwa hospital ili kupatiwa matibabu na kwamba vikao hivyo awali vilipangwa kusikiliza kesi tano za mauaji kuanzia tar 6 nov hadi 17 novemba 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad