HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 1, 2017

KINONDONI YAIPONGEZA HAZINA KWA KUONGOA DAR

Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni, Kiduma Mageni akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Hazina, Emma James kwenye mahafali ya shule hiyo. Anayefuata ni Mkuu wa shule hiyo, Patrick Cheche.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Hazina wakionyesha moja ya michezo yao kwenye mahafali ya shule hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Ofisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Kiduma Mageni.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Hazina iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam , wakiwa kwenye shindano ya kujibu maswali ya papo kwa papo wakati wa mahafali ya shule hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Ofisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Kiduma Mageni

Na Mwandishi Wetu
WILAYA ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imeelezea siri ya kuwa ya kwanza kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, huku ikiipongeza shule ya Hazina ambayo imekuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Dar es salaam.

Ofisa Elimu Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni, alisema jana kuwa matokeo hayo ni matunda ya ushirikiano mzuri baina ya viongozi wa Wilaya hiyo, wamiliki wa shule, walimu na wanafunzi.

Alisema hii ni mara ya kwanza kwa Wilaya yake kuwa ya kwanza kitaifa na kwamba hata kiwango cha ufaulu walichofikia hawakuwahi kukifikia hivyo ni mafanikio ya kujivunia.

“Haya ni matunda ya ushirikiano wetu, tunafanyakazi kama timu moja kuanzia wazazi, uongozi wa Wilaya, kata, uongozi wa shule hivyo tunaahidi kuendelea na ushirikiano huu na mimi kama kiongozi wa elimu wa Wilaya nitahakikisha tunazidi kuwa juu,” alisema

Aliipongeza shule ya Hazina kwa kushika nafasi ya kwanza kwa Wilaya ya Kinondoni, wa kwanza Mkoa wa Dar es salaam kwa kundi la shule zenye zaidi ya wanafunzi 40 na vile vile kushika nafasi ya saba kitaifa.

Alisema shule za umma nazo zimefanya vizuri sana kwenye matokeo hayo ingawa zilikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi huku akisifu mpango wa elimu bure kuwa chachu ya mafanikio hayo.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Patrick Cheche, alisema kwa miaka zaidi ya 10 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo wamekuwa wakipata mafanikio makubwa mwaka hadi mwaka kwenye matokeo ya kitaifa.

Alitoa mfano kuwa shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kitaaluma kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na hadi Taifa na kumekuwa na mabadiliko channya kila mwaka ambapo mwaka huu imefanikiwa kuongoza wilaya ya Ilala, nafasi ya kwanza mkoa na nafasi ya saba kitaifa.

Alisema wamefanikiwa kufungua shule nyingine maeneo ya Bunju ijulikanayo kama New hazina ikiwa ni mipango yao ya kuboresha elimu kuendana na malengo ya millennia.

Cheche alisema malengo yao ni kuendelea kufundisha kwa bidii sana ili kuendelea kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa na kusaidia watoto wengi wa Tanzania kupata elimu bora.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad