HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 23 November 2017

KATIBU TAWALA KISHAPU AKABIDHI HATI ZA KIMILA ZA ARIDHI KWA WANANCHI

Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ikishirikiana na Shirika la Misaada ya Kijamii (REDESO) imekabidhi hati 43 za kimila za ardhi kwa wananchi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge.
Hati hizo zimekabidhiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese kwa wananchi hao ikiwa ni sehemu ya jumla ya hati 87 ambazo zinatarajiwa kutolewa katika kijiji hicho.
Kengese aliwataka wananchi hao kuzitumia hati kwa kuboresha hali zao kiuchumi kwa kukopa katika taasisi za kifedha na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kujipatia kipato.
Alisisitiza kilimo chenye tija katika ardhi hizo ambapo aliwataka kufuata kanuni bora za kilimo ili kupata mavuno kwa kiasi kikubwa ambapo wataipa thamani ardhi wanayomiliki.
Aidha, alisema pamoja na hayo pia wananchi wanapaswa kupanda miti ili kutunza mazingira kwani ardhi iliyotunzwa kwa kupandwa miti ina thamani kubwa zaidi ya ile isiyokuwa na mti hata mmoja.
Kwa upande mwingine Katibu Tawala huyo aliwataka wananchi waliokabidhiwa hati hizo kuwahamasisha wanajamii wenzao kuona umuhimu wa kupata hati za kimila za kumiliki ardhi katika maeneo yao.
 Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese akizungumza na wananchi wakati wa zoezi la kukabidhi hati za kimila katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge.
 Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese akikabidhi moja ya hati za kimila kwa mwananchi katika kijiji cha Negezi.
 Meneja wa na Shirika la Misaada ya Kijamii (REDESO), Charles Buregeya akionesha moja ya hati miliki za kimila kwa wananchi waliofika kwa ajili ya kukabidhiwa kijiji cha Negezi.
 Afisa Mipango Miji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Celestine Mwizarubi akitoa malekezo kuhusu hatua za utoaji wa hati za kimila wakati wa hafla ya makabidhiano.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu akitoa neno wakati wa hafla hiyo.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese akikabidhi hati ya kimila kwa mwananchi katika kijiji cha Negezi.
 Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese (wa pili kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika wa hati za kimila na maafisa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad