HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 10, 2017

DStv inakuletea chaneli maalum itakayoonyesha Tuzo za AFRIMA 2017

Wateja wa DStv wamepata nafasi ya kushuhudia Tuzo kubwa Afrika zinazotoa heshima na kutambua mchango wa wasanii kutoka Afrika,  kimataifa.

Ni Tuzo za AFRIMA (The All Africa Union Music Award channel) ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapili hii na DStv imekuletea chaneli maalum kwa ajili ya kuonyesha matukio yote muhimu na utoaji wa Tuzo hizi.

Chaneli hii imeanza  kuanekana kuanzia Novemba 9 na inapatikana kwa wateja wote wa DStv kupitia namba 198 iliyopo kuanzia kifurushi Bomba cha sh.19,000 tu. Kwa kipindi cha siku tatu mfululizo,  wateja wa DStv watafurahia burudani kadha wa kadha kutoka kwa wasanii waliochaguliwa kwenye Tuzo hizi ikiwemo matamasha mbali mbali ya ndani na nje ya Bara  la Afrika kutoka kwa wasanii hawa.

Ni wakati wa watanzania  kushuhudia wasanii wetu wakipokea Tuzo zao za kimataifa  LIVE kupitia DStv pekee, Lipia Kifurushi chako cha DStv sasa kuanzia kifurushi Bomba kwa sh.19,000, ili usipitwe na Tuzo hizi.

Majina ya wasanii kutoka Tanzania na vipengele walivyochaguliwa ni:

Best Female Artist in Eastern Africa

Lady Jaydee – Sawa na Wao
Nandy- One Day
Feza Kessy - Walete
Vanessa Mdee- Cash Madame

Best Male Artist in Eastern Africa

Ali Kiba – Aje
Diamond Platnumz – Eneka
African Fans Favorite
Darassa- Muziki

Best African Collaboration

Ali Kiba ft. MI – Aje

Best Artiste/ Group in African Contemporary

Ali Kiba ft. MI – Aje

Best Artist in African Pop

Diamond Platnumz- Eneka

Best Artist / Group in African R n B & Soul

Ali Kiba – Aje

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad