HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 25 November 2017

DK.NDAZI - UCHUMI WA VIWANDA NCHINI KUTATUA TATIZO LA AJIRA

Na Chalila Kibuda
KUANZISHWA kwa viwanda nchini kutatua tatizo la ajira kwa watu wenye mafunzo Stadi kutokana na serikali kuwa na dhamira ya dhati katika kwenda katika uchumi wa viwanda nchini.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo, Stadi (VETA), Mhadisi Dk. Bwire Ndazi wakati Mahafali ya 47 ya Chuo cha Chang’ombe VETA jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa vijana wanaohitimu katika Chuo cha Chang’ombe  kutokana na mafunzo stadi wanayoyafanya watakwenda katika soko la ajira.
Ndazi amesema kuwa tatizo la ajira sio kwa Tanzania ni dunia nzima hiyo inatokana na ongezeko  la idadi ya watu katika kila nchi hivyo kila mtu lazima awe mbunifu katika kuweza kuendana na mahitaji ya soko la ajira.
Aidha amesema kuwa wahitimu lazima watumie vipaji vyao ikiwa ni pamoja na kijiajiri kwa mfumo wa kikundi ambapo Halmashauri zina mipango katika uwezeshaji wa vikundi.
Amesema suala la changamoto ya walimu, Mamlaka inatarajia kuajiri walimu 90 hivyo VETA Chang’ombe nayo itaweza kupata walimu hao lakini sio kwa kumaliza tatizo.
Nae Mkuu wa Chuo cha Chang’ombe, Douglas Kipokola amesema kuwa Chuo kinachangamoto za walimu ikiwa ni pamoja ya walimu kupata mafunzo katika sehemu mbalimbali ili kuweza kuendana na teknolojia.
Amesema kuwa kwa mwaka huu wameweza kuhitimu zaidi ya 11000 wa kozi fupi pamoja na kozi ndefu ambao sasa ndio mabalozi wa kutangaza mafunzo yanayotolewa na VETA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo, Stadi (VETA), Mhandisi Dk. Bwire Ndazi akizungumza katika mahafali ya 47 ya Chuo cha VETA Chang’ombe yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam, Habib Bukko akizungumza juu Chuo cha Chang’ombe jinsi kinavyozalishwa wahitimu ambao wanaweza kujiajiri au kuajiriwa.
Mkuu wa  Chuo Cha Chang’ombe  VETA, Douglas Kipokola akitoa taarifa ya Mahafali ya 47 chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elmu ya Mafunzo, Stadi (VETA), Mhadisi Dk. Bwire Ndazi akimkabidhi cheti  Mhitimu wa Kozi ya Upambaji , Zuhura Hamis katika mahafali ya 47  ya Chuo cha Chang’ombe  VETA.
Sehemu ya wahitimu wa Chuo cha VETA, Chang’ombe wakisikiliza hotuba mbalimbali katika mahafali ya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi katika mahafali ya Chuo cha VETA, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad