HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 9 November 2017

Citibank yafungua Makao Makuu Mapya Tanzania


Wakikata ribbon/utepe katika uzinduzi wa ofisi mpya za CitiBank jijini Dar es salaam, Mgeni Rasmi Mr. John Rubuga - Commissioner of External finance katika wizara ya Fedha na mipango, pamoja na CEO wa CitiBank(Europe, Middle East and Africa)- Jim Cowles, na Bi. Inmi Patterson anaekaimu nafasi ya Balozi wa Marekani Tanzania (charge d' affaires) na viongozi mbalimbali wa ngazi za Juu wa Citi kutoka Europe, Middle East & Africa.


Citibank Tanzania ambayo ni benki chini ya makampuni ya Citigroup Inc. iliyojikita katika utoaji wa huduma za kifedha duniani kote, jana ilifungua rasmi Makao Makuu Mapya katika jengo lililopo kitalu namba 1962, barabara ya Toure huko Oysterbay karibu kabisa na ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.


Akiongea katika ghafla fupi ya uzinduzi wa jengo hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo kwa bara la Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, Jim Cowles, alisema “ Mtazamo na mwelekeo wa benki ya Citi ni kuwa benki bora inayohudumia wateja wake kwa usalama mkubwa huku ikiinua uchumi na kukua kwa ufanisi. “Uwekezaji huu mkubwa katika jengo letu jipya ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma bora za kifedha katika nchini.”

Citi inafanya kazi duniani kote huku ikizingatia kutoa huduma kwa wateja na washirika wake kwa kupanua wigo wa huduma na uchumi hasa katika kuendeleza masoko ya kifedha katika maeneo yaliyo dhaifu. Benki hii ilianza kutoa huduma zake nchini Tanzania mwaka 1995 katika jiji la Dar es Salaam ikiwa imejikita katika wateja wa makampuni na wawekezaji.

“Kwa miaka miwili sasa benki ya Citi imekuwa ikichangia huduma za kifedha nchini Tanzania huku ikiwa inaongoza kwa kuwa na mtandao wa matawi zaidi ya 160 ikihudumia wateja wa aina zote ikiwemo taasisi za kifedha’, alisema Joseph Carasso, ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Citi nchini Tanzania.

Mgeni rasmi, Bwana John Rubaga, Commissioner External Finance, kwa niaba ya Mheshimiwa Dr. Phillip I. Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango, alisema, “Serikali ina heshima kubwa kushiriki katika ghafla hii na inajisikia fahari kuona benki ya Citi ikiongeza tena uwekezaji na kuiweka nchi hii katika ramani yake ya mtandao wa zaidi ya nchi 160 duniani kote. Huu ni uthibitisho rasmi kuwa Tanzania inajiweka katika huduma za kifedha kuboresha maisha ya wananchi wake kupitia huduma za kifedha zinazotolewa na mabenki zinazoongezeka.”

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wananchi na maofisa wakubwa wanaofanya kazi katika mabara ya Ulaya, Mashariki ya kati na Afrika, wakiwemo Peter McCarthy ambaye ni Afisa mtendaji wa huduma, Jenny Grey ambaye ni Afisa mkuu rasilimali watu, Mdhibiti wa mahesabu ya ndani Andrew Blight na Afisa Mtendaji Mkuu wa Citibank katika nchi za Afrika Mashariki Joyce-Ann Wainaina.


Citibank Tanzania ni benki ya nane kwa ukubwa nchini na imweshawahi kutwaa tuzo ya Uwekezaji nchini na Afrika kutoka Ulaya na tuzo ya miamala ya kifedha barani Afrika.

Wakifungua Jiwe la msingi katika ofisi mpya za CitiBank zilizofunguliwa maeneo ya Oysterbay jijini Dar es salaam Mgeni Rasmi Mr. John Rubuga, CCO ( Chief Commercial Officer) wa CitiBank Mr. Joseph Carasso na viongozi wengine waliokuwepo katika hafla hiyo.
Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Mr. John Rubuga akiwa na viongozi mbalimbali walioalikwa katika ufunguzi wa ofisi mpya za CitiBank zilizopo jirani na ufukwe wa Coco Oysterbay Jijini Dar es salaam,

CitiBank CEO (Europe, Middle East & Africa) Mr. Jim Cowles akizungumza na wageni waalikwa, wafanyakazi wa CitiBank pamoja wa watu mbalimbali waliohudhuria ufunguzi huo wa ofisi mpya za CitiBank.

Wageni mbalimbali na washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad