HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 20 November 2017

CCM Z'BAR YATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KIFO CHA MWANAHABARI WA ZBC

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimepokea kwa mshituko na huzuni mkubwa taarifa ya kifo cha Mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Marehemu Maridadi Aman kilichotokea jana katika Hospitali ya Tasakhtaa Grobal, Vuga Zanzibar.

Kutokana na msiba huo mzito kwa Tasnia ya Habari nchini, CCM Zanzibar inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa marehemu enzi za uhai wake alikuwa mstari wa mbele katika kutangaza taarifa za Chama Chetu kwa jamii.

Tunaamini kwamba juhudu, maarifa na busara za marehemu Maridadi zitabaki kama kumbukumbu na muongozo wa kuongeza hamasa ya kujituma kiutendaji kwa Wanahabari wote nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi anawapa pole Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Wanahabari wote, ndugu wa familia pamoja na walioguzwa na msiba huo.

Mpendwa wetu ametangulia mbele ya Haki , ataendelea kubaki katika kumbukumbu zetu daima na tunamuomba Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi Amin.

Imetolewa na:-

NDG.WARIDE BAKAR JABU

KATIBU WA KAMATI MAALUM WA NEC,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI CCM -ZANZIBAR,
20, NOVEMBA 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad