HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 12 November 2017

ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI KWENYE HALMASHAURI

NA KAROLI VINSENT
SERIKALI imeshauriwa kuwaongeza Maafisa Ugani kwenye halmashauri mbalimbali nchini ili waweza kumsaidia  Mkulima  aweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi .
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa Kilimo (ANSAF), Audax Rukongwe wakati wa mkutano uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Kilimo kujadili kuhusu huduma za Ugani kwa kulima ili ziendane na shughuli ya Viwanda hapa nchini.

Amesema  kitendo cha sasa cha kumtumia Afisa Mgani mmoja katika Kijiji kimoja  ni kitendo ambacho hakiwezekani katika kumsaidia Mkulima.
“Afisa Ugani katika Kijini Kimoja, ni kitu hakiwezekani,maana leo tunasema tuna kijiji kimoja na kesho tukawa na vijiji ishirini hivyo itashindikana kwa afisa Ugani huyu kufanya kazi kwenye vijiji vyote, ni vema serikali ikaliangalia hili”Amesema Rukongwe.

Amesema  kutokana na hali ilivyo ya uchache wa Maafisa Ugani kunahaja ya sekta binafsi kuwekeza kwenye utoaji wa Huduma ya  Ugani kwa Wakulima  ili iwe rahisi kwa Mkulima kusaidika.


“Sasa kuna haja sekta binafsi kuwekeza kwenye kutoa huduma ya Ugani  kwa wakulima ili waweze kulipia kwa kiasi husika cha fedha, kwa mfano kwa wale wakulima wafugaji kama Ngome anaumwa Nyumbani hanahaja ya kumsubili aje Afisa Ugani bali anamtafuta Afisa ugani  wa Sekta Binafsi anampa hela anamsadia “Amesema Rukongwe. 
Kwa Upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokine (SUA)Dk Sizya Lugeye ambaye ni miongoni wa wadau hao katika mkutano huo, ameishauri serikali kuhakikisha wanawaongezea nguvu za maafisa Ugani waliopo ikiwemo kuwapata fedha pamoja vitendea kazi ili waweze kufanya kazi kwa ufanizi zaidi katika kuwahudumia wakulima.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa Kilimo, Audax Rukongwe akizungumza na Waandishi wa habari leo wakati wa Mkutano wa wadau wa Kilimo ili kujadilia masuala mbalimbali yanahusu Kilimo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad