HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 2 October 2017

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA ILIVYOFANA BENKI YA CRDB TAWI LA KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM.

BENKI ya CRDB tawi la Kariakoo lasherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo inafanyika kila mwaka kwa wiki nzima kuanzia leo Oktoba 2 hadi Oktoba 6,2017.


Akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa wateja, Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo jijini Dar es Salaam leo amesema wiki hii ni wiki ya huduma kwa wateja na ni wiki ya kuwahudumia wateja pamoja na kuwahamasisha wateja wajitokeze kufungua akaunti katika benki hiyo katika tawi la Kariakakoo jijini Dar es Salaam.

Amesema wateja ambao hawana akaunti katika benki hiyo waende wakafungue ili kuweza kujipatia huduma kedekede zilizopo katika benki hiyo ikiwa pamoja na kujipatia mikopo.


Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo akizungumza na wateja wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuwashukuru pamoja na kuwaomba kufungua akaunti za benki katika Tawi hilo kwani wanatoa mikopo mbalimbali katika tawi hilo. Wiki ya Huduma kwa mteja huadhimishwa kila mwaka kwaajili kusherekea pamoja na kuwahudumia wateja wao inavyopaswa.
 Baadhi ya Wateja wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo wakifungua Shampeini kwaajili ya kusherekea pamoja wiki ya huduma kwa wateja ambalo huadhimishwa kila mwaka.
 Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo akimiminiwa Shampeni na Mteja wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam mapama hii leo.
  Mteja wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo akiwamiminia shampeni baadhi ya wateja pamoja na wafanyakazi wa Benki hiyo ikiwa ni Kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.
 Keki ya Wiki ya huduma kwa wateja benki ya CRDB tawi la Kariakoo.

 Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo wakigonganisha glasi za shampeni kwaajili ya kudherekea wiki ya huduma kwa mteja ambayo huadhimishwa kila mwaka.
  Mteja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Abdul Malambo(Kulia) akikata keki kwaajili ya Kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa Mikopo benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Brigitha Barthalome akimsaidia mteja kukata kata vipande vya keki mteja Abdul Malambo wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka. 
 Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo akimlisha keki mteja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Abdul Malambo wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo ambayo hufanyika kila mwaka.
Mteja wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo akimlisha keki Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo ikiwa ni kusherekea ufunguzi wa wiki ya huduma kwa mteja jijini Dar es Salaam leo.


 Mfayakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo akimlisha keki Mteja jijini Dar es Salaamleo ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila mwaka.
 Baadhi ya wateja wa beki ya CRDB tawi la Kariakoo wakiwa katika benki hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka.
 Baadhi ya wateja wakijaza fomu za kuweka pesa na kuchukua pesa katika benki ya CRDB tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. 

 Wateja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo wakilishwa keki ikiwa ni kuadhimisha ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.


Wateja na wafanyakazi wa beki ya CRDB tawi la Kariakoo wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad