HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 2 October 2017

Mawakala wa mashindano ya urembo wabanwa

Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Limited inayoandaa mashindano ya Mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania) kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa nchini (Basata) imefanya marekebisho ua Kanuni, Sheria na Taratibu za mashindano ya urembo nchini.

Marekebisho hayo yamefanywa ili kuyafanya mashindano ya Miss Tanzania nchini kuwa bora zaidi na kuondoa changamoto ambazo wadau wake wamekuwa wakizipata.

Afisa Habari wa Lino Internationa Agency Limited, Hidan Ricco amesema kuwa kutokana na kuwa katika mchakato wa kuandaa na kukamilisha taratibu hizo mpya, wamesabisha kuchelewa kupata kibali kutoka Basata cha kuanza mchakato wa mashindano ya mwaka huu ya Miss Tanzania.

Ricco alisema kuwa wapo mawakala ambao tayari wamefanya mashindano na wengine ambao wanakusudia kufanya mashindano na vile vile wapo wengine ambao waliteuliwa kwa mujibu wa sheria ambazo wanatakiwa kuzifuata kabla ya kufanya shindano.

Aliyataka masharti hayo kuwa ni pamoja na kusajiliwa na kulipa ada ya Basata, kukabidhi zawadi za washiriki wote siku 14 kabla ya shindano kwa afisa utamaduni wa ngazi husika na vile vile kutoa taarifa siku saba baada ya mashindano.

“Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Kimited hautosita kuchukua hatua za kinidhamu kwa wakala ambaye atashindwa kufuata kanuni, sheria na taratibu za mashindano ikiwa amoja na shindano husika,” alisema Ricco.

Aliwaomba waandaaji (mawakala) kuzingatia mashari hayo ambao lengo lake ni kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakisababisha malumbano mbalimbali miongoni mwa wadau na kampuni yao kunyooshewa kidole.

“Tunasisitiza, wakala ambaye atakwenda kinyume na taratibu zetu atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa pamoja na kutotambua shindano lake, hivyo ni wajibu wa wakala kuhakikisha anafuata taratibu hizi kwa lengo la kuboresha mashindano,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad