HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 15, 2017

WAZIRI WA VIWANDA NA UWEKEZAJI, MWIJAGE AMEWATAKA KAMPUNI YA DANUBE HOME NA GSM KUENDELEA KUWEKEZA NCHINI

Muonekano wa nje wa duka la Danube Home lililozinduliwa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Uwekezaji  Charles Mwijage akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wateja waliojitokeza katika uzinduzi wa duka la Danube Home jana  Mlimani City na kuwataka wamiliki wa duka hilo kutumia malighafi zinazopatikana nchini kwani zina ubora wa hali ya juu, Kulia ni Mkurugenzi wa GSM Ghari Said Mohamed na kushoto ni Mkurugenzi wa Danube Home Adel Sajan.
Balozi wa Danube Home, Zarina Hassan akizungumza baada ya uzinduzi wa duka la Danube Home na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kwenye duka la lao kwa ajili ya kujipatia bidhaa zenye ubora na thamani nafuu.

 Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage akipata  maelekezo wakati alipotembelea maeneo mbalimbali ndani ya duka la Danube HomeMlimani City jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage akitembelea maeneo mbalimbali ndani ya duka la Danube Home baada ya ufunguzi jana Mlimani Cit, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Danube Home Adel Sajan na Mkurugenzi wa GSM Gharib Said Mohamed pamoja na Balozi wa Danube Home Zarina Hassan.
  Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage akikata utepe kuzindua duka la Samani lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.

 Baadhi wa wateja waliojitokeza katika ufunguzi wa duka la Danube Home wakiwa wanaangalia baadhi ya bidhaa zinazopatikana kwenye duka hilo jana Jijini Dar es salaam.

 WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage amewataka kampuni ya Danube Home na GSM kuendelea kuwekeza nchini kwani wanaposema uchumi wa viwanja ni pamoja na biashara za samani kama wanazojishughulisha nazo.

Mwijage ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa duka la Danube Home uliofanyika jana Mlimani City pamoja na kutambulishwa kwa balozi wa Danube nchini Tanzania Zarina Hassan.

Akizungumza baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya duka hilo, Mwijage amesema kuwa anatarajia kuona Danube wanatumia malighafi zinazopatikana nchini kwa ajili ya kutengenezea samani mbalimbali za ndani ikiwemo masofa, vitanda na zinginezo kwani zinapatikana kwa urahisi.

"Natarajia kuona mnatumia samani zinazopatikana nchini, pia nimesikia hapa mkisema katika maandalizi ya kufungua duka hili mmewatumia zaidi watanzania na hicho ni kitu kizuri na ninaamini mtaendelea kuwaamini watanzania",amesema Mwijage.

Mkurugenzi wa Danube Home Adel Sajan amewashukuru watanzania kwa ukarimu mkubwa waliokuwa nao na zaidi Tanzania ni eneo salama kwa ajili ya kufanya biashara kwani kwa kushirikiana na kampuni ya GSM wameweza kufungua duka la tatu.

Kampuni ya GSM na Danube Home zimeweza kutoa ajira zaidi ya 1000 kwa nchini huku aslimia 99 wakiwa ni watanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad