HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 15, 2017

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, ULEGA AMEWATAKA WAKULIMA NA WAFUGAJ IWAPENDANE

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega ambaye ni Mbunge wa Mkuranga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyanduturu akiwa ni ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake kuwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega  amewataka wakulima na wafugaji wa vijiji vinne alivyotembelea vya  wilaya ya Mkuranga kuondokana na tofauti zao na badala yake wapendane.

 Hayo aliyasema katika ziara yake kwa wananchi wa jimbo lake la Mkuranga-Pwani ambapo aliweza kuelezwa kero mbalimbali na kuahidi kuzishughulikia.

Katika ziara hiyo pia aliweza kuchangia jumla ya fedha kiasi cha shilingi Mil.6 pamoja na mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati zilizomo katika vijiji hivyo.

Aidha pia amewaomba wananchi kuunda vikundi mbalimbali vya ujasiriamali hususani ufugaji wa kuku samaki na mifugo mbalimbali  ili kuwawezesha kuondokana na umaskini.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia ujenzi wa jengo la zahanati ya kijiji cha Nyanduturu  kata ya Nyamato ambayo pia amechangia Milioni moja na nusu pamoja na saruji 50 ili kufanikisha ujenzi huo unaoendelea.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wakazi Wa kijiji cha Mvuleni kata ya Nyamato wakati wa ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake katika wizara hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ambapo aliwachangia Shilingi milioni moja na nusu pamoja na mifuko 50 ya saruji kufanikisha zahanati inayojengwa kijijini hapo.
 Mwenyekiti wa kijiji cha Mvuleni,Mohammed Mpunjika akimkabidhi risala yao Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alipofanya ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
 Naibu Waziri  wa Mifugo na Uvuvi ,Abdallah Ulega akisalimiana na wazee wa kijiji cha Mvuleni jana alipofanya ziara yake ya kwanza kijijini hapo.
 Mmoja wa akina mama kutoka katika kijiji cha Tipo kata ya Nyamato akiuliza swali kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wakati alipofanya ziara yake 
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga,Ally Mohammed akizungumza jambo.
 Naibu Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiteta jambo na baadhi ya wamasai ambao ni wafugaji katika kijiji cha Kifumangao kabla ya mkutano wake kuanza hapo jana.
 Naibu Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa katika jengo linalojengwa la zahanati ya Kifumangao ambapo ametoa zawadi ya fedha miliono moja na nusu pamoja na saruji mifuko 50. Jana katika ziara yake hiyo kwa vijiji vinne amechangia jumla ya mifjko 200 ya saruji pamoja na jumla ya fedha milioni sita.
 
Muonekano wa jengo hilo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad