Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo akieleza kuhusu utendaji wa taasisi anayoiongoza wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
Afisa kutoka Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) akiwasilisha mada kuhusu kazi na mafanikio ya wakala wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) katika wakala hiyo mapema leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifuatilia mada iliyowasilishwa kuhusu kazi na mafanikio ya TaGLA alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan P. Mlawi, na Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa TaGLA, Bw. Charles Senkondo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Watumishi wa TaGLA mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipata maelezo kuhusu mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi wakati wa mikutano ya kieletroniki (Video Conference) katika ofisi za TaGLA wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea taarifa (nakala ngumu na laini) zenye shughuli zinazofanywa na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw. Charles Senkondo baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika wakala hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokewa na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma alipofanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kazi katika ofisi za Bodi hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald Ndagula akitoa neno la shukurani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) mara baada ya Waziri kumaliza kuzungumza na watumishi wa bodi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akijionea utunzaji wa kumbukumbu alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Idara ya Kumbumbuku na Nyaraka za Taifa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea nyaraka mbalimbali zinazohusu utunzaji wa kumbukumbu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Charles Magaya katika ofisi za Idara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma imeagizwa kufanya
utafiti wa kina utakaowezesha kuwa na uwiano sawa wa malipo ya mishahara
na masilahi ya watumishi wote serikalini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Kapteni (Mstaafu), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema hayo leo
wakati wa ziara ya kikazi katika Ofisi za Bodi ya Mishahara na Masilahi katika
Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mkuchika amesema kuna baadhi ya taasisi/Idara za Serikali zinalipa
watumishi wake mishahara mikubwa tofauti na taasisi nyingine jambo ambalo
limekuwa likisababisha watumishi kutotulia sehemu moja na kutafuta masilahi
bora zaidi sehemu nyingine.
“Hii haiwezekani, mmesoma darasa moja, fani moja na mko cheo kimoja, lakini
mnalipwa mishahara tofauti wakati serikali ni moja, ni lazima mlifanyie utafiti
wa kina suala hili. Masilahi ya watumishi wa umma lazima yawe sawa” Waziri
Mkuchika amesisitiza na kuongeza kuwa kumekuwa na malalamiko mengi
serikalini kuhusu tofauti kubwa ya mishahara miongoni mwa watumishi wa
Serikali Kuu na baadhi ya taasisi za serikali.
Aidha, Mhe. Mkuchika amewataka watumishi wa Bodi hiyo kuwa wabunifu na
kupendekeza mambo ambayo yatawavutia Watumishi wa Umma kufanya kazi
Serikalini kwa dhati kwa kuzingatia taaluma zao na mgawanyo wa majukumu.
“ Kila mtumishi ana taaluma yake na mgawanyo wa majukumu aliyopewa
wakati anaanza kazi, hivyo ni vema kila mtu akazingatia hayo ili kuwa na
utendaji bora serikalini,” Mhe. Mkuchika amesema.
Mhe. Mkuchika, ameendelea na ziara ya kikazi ya kujitambulisha na kujifunza
kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake, ambapo leo
ametembelea Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bodi ya
Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa.
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma ni matokeo ya Tume
ya Rais ya Malipo ya Mishahara ya mwaka 2006 iliyopewa jukumu la kuishauri
Serikali namna ya kuboresha malipo ya mishahara na motisha nyingine katika
Utumishi wa Umma.
No comments:
Post a Comment