HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 9, 2017

WAPENI WATOTO FURAHA YA MAISHA KWA KADI ZA NHIF:MAKINDA

 Meneja wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki  akiendelea kutoa maelezo ya umhimu ya mfuko huo kwa baadhi ya waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.
 Spika Mstaafu na Mwenyekiti  wa Bodi wa Mfuko  ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda , akizungumza na baadhi ya waumini baada ya kumaliza uzinduzi wa huduma ya “TOTO AFYA KADI” katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.
 Spika Mstaafu na Mwenyekiti  wa Bodi wa Mfuko  ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda, akizungumzia umhimu wa kutumia NHIF wakati wa uzinduzi wa huduma ya “TOTO AFYA KADI” katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.

Bbaadhi ya waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.

SPIKA Mstaafu na  Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko  ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda  azindua huduma ya “TOTO AFYA KADI” kwenye nyumba za ibada.

Akizungumza na waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge amesema  huduma hiyo itatolewa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 kwa  Sh. 50,400 kwa mtoto mmoja kwa mwaka.

Makinda amesema kampeni hizo ambazo zitaendelea kwenye Madhehebu ya Dini lengo ni kuwa rafiki na huduma hiyo ili kufikia mwaka kesho watanzania asilimia zaidi ya  80 wawe wamejiunga na huduma hiyo.

Makinda amesema kiasi hicho  cha Sh. 50,400 kitakachochangiwa kwa mwaka kitamuwezesha mwanachama huyo kupata matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

Naye Meneja wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki amesema fao hilo pia hutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu kwa Sh. 50,400.

Pia amesema NHIF hutoa huduma kwa vikundi vya  wajasiriamali walio kwenye vikundi vya watu kuanzia 10 kwa Sh. 76,800  kwa kila mwanachama mmoja ambaye atachangia fedha hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad