HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 2, 2017

WADAU SEKTA YA ARDHI WAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MIFUMO

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendesha warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa masuala ya sekta ya ardhi nchini kuhusu mifumo mbalilmbali inavyotumika katika kutoa huduma kwa wananchi.

Akifungua warsha hiyo Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt. Moses Kusiluka alisema, hadi sasa wizara inatumia mfumo zaidi ya mmoja kutoa huduma za kila siku kwa mwananchi. Uwepo wa mifumo hiyo katika utoaji huduma za sekta ya ardhi ni muhimu kwa ajili ya kurahisisha huduma. Ili kufikia malengo, ni lazima kuwepo na mfumo mmoja utakaounganisha mifumo yote hiyo kwa lengo la kuongeza ufanishi na kuboresha huduma.

Uundaji wa mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (Intergrated Land Management Information System, ILMIS) unatekelezwa na Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishiriana na wataalamu kutoka kampuni ya IGN FI kwa udhamini wa Benki ya Dunia. Uundaji huu ulishaanza na kwa sasa mfumo uko katika hatua ya majaribio.

Dhumuni kuu la uundaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi ni kuimarisha usalama katika umiliki wa ardhi kwa kuboresha usahihi katika taarifa za ununuzi ardhi, usajili, upimaji na pia katika kusimamia ardhi kwa ujumla wake.

Utekelezaji wa Mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS), utahusisha mambo mbalimbali kama vile njia rahisi na rafiki ya kusimamia uundaji na uendelezaji wa mfumo wenyewe, majaribio ya mfumo katika utekelezaji, ubadilishaji wa taarifa za ardhi zilizopo mfano taarifa za upimaji na ramani, hatimilki na kuziweka katika mfumo.

Naye Msajili Msaidizi wa Hati, Appolo Laizer alisisitizia umuhimu wa utumiaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS) kwa wadau wa sekta ya ardhi alipokuwa akielezea jinsi hatimilki zitakavyotolewa na mfumo huo.

Alisema, utoaji wa hati kupitia mfumo utaongeza usalama katika nyaraka za umiliki, huduma sahihi, salama na kwa unafuu zaidi. Mfumo utapunguza muda wa kuhakiki taarifa katika uhamisho wa milki kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kuongeza ulinzi kwenye maeneo yaliyotengwa kama hifadhi ya barabara, misitu au maeneo ya wazi.

Utoaji wa hatimilki kwa kutumia mfumo utasaidia sana kupunguza kama sio kumaliza kabisa migogoro ya ardhi kwa kulinda umiliki wa mwananchi. Pia mfumo utaondoa migogoro ya umilikishaji wa hati kwa mtu zaidi ya mmoja pamoja na kuongeza ulinzi wa hatimilki katika taasisi za kifedha.
 Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitoa ufanunuzi juu ya ujenzi wa Mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya Ardhi (ILMIS).
 Wadau wa Sekta ya Ardhi wakisiliza taarifa kuhusu mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya Ardhi nchini kutoka kwa mtaalamu (hayuko pichani).
Wadau wa masuala ya sekta ya aAdhi wakiwa katika picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad