HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 18, 2017

VODACOM YAMKABIDHI MKWANJA WAKE SHAFIK BATAMBUZE WA SINGIDA UNITED

 Meneja wa chapa wa Vodacom Tanzania,Yvonne Maruma(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya Tsh.Milioni moja mchezaji bora wa mwezi septemba,Shafik Batambuze wa timu ya Singida United inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Katikati ni Afisa Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo, Ibrahim Kaude.
Mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi Septemba wa Singida United, Shafik Batambuze akiwa ameshikilia hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni moja baada ya kukabidhiwa rasmi na wadhamini wakuu wa ligi kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi huo.

Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC,Ambao ndiyo wadhamini wa ligi kuu Tanzania bara, Jana wamemkabidhi mchezaji bora wa ligi kwa  mwezi septemba wa Singida United,Shafik Batambuze hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1/- kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi huo.

Akimkabidhi hundi hiyo Meneja wa Chapa wa kampuni hiyo,Yvonne Maruma alisema kwa mjibu wa taratibu unaofanywa na kamati ya Tuzo ya VPL iliyopo chini ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Vodacom ikiwa kama mdhamini mkuu haina budi kutekeleza matakwa yote yale yaliyopo katika mkataba na kuweza kutoa kitita cha shilingi milioni 1/-kwa mchezaji bora wa kila mwezi ikiwa na lengo la kuwapa motisha wachezaji wote wanaoshiriki ligi kikuu,Alisema Maruma.

“Kwa mjibu wa wa kikao cha kamati ya Tuzo ya VPL imeonesha kwamba mchezaji huyu alitoa mchango mkubwa kwa singida united kupata pointi 10 katika michezo mine,ambayo timu yake ilicheza kwa mwezi huo,matokeo ambayo yaliiwezesha Singida United kutoka nafasi ya 10 katika msimamo na kupanda hadi nafasi ya nne kwa mwezi huo wa Septemba,Singida United ndiyo timu iliyokusanya alama nyingi kwa mwezi huo ukilinganisha na timu nyingine 15 zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara”,Alisema Maruma

Kwa upande wake Sharif Batambuze,aliishukuru kamati ya tuzo ya ligi na wadhamini wakuu kwa kumpatia fedha hizo na kusema atazitumia vizuri ili iwe kumbukumbu nzuri katika maisha yake kwa msimu wa 2017 Batambuze.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad