HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 2 October 2017

UDHALILISHAJI WA WANAWAKE KATIKA MITANDAO YA KIJAMII WAPINGWA NA UMOJA WA WANAWAKE WANASIASA.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
UMOJA wa Wanawake wa Wanasiasa (WCP-Ulingo) umesema  wanawake wamekuwa wanadhalishwa utu wao katika mitandao ya kijamii Si michuzi Media na kutaka vyombo vya dola kuchukua hatua dhidi ya wanaofanya hivyo.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Sekretarieti ya Umoja huo, Angelina Mtahiwa amesema kuna uovu unafanywa baadhi ya mitandao ya kijamii katika kuwachafua wanawake katika nafasi zao hali ambayo inarudisha nyuma wanawake kuogopa kujihusisha masuala mbalimbali kwa jamii.

Amesema mitandao ya jamii itumike katika kujenga nchi kuelimisha  masuala ya kijamii ili nchi iweze kusonga mbele kiuchumi pamoja kuwatoa  wanawake katika kushiriki nafasi mbalimbali sio kutumika katika mitandao kwa ajili ya kudhalilishwa.

Nae Mjumbe wa Sekretarieti hiyo, Swaum Rashidi amesema kwa sasa wanawake wamekuwa wakishiriki shughuli za kuchumi , siasa, biashara  na kuwa sehemu ya mchano katika kuchangia maendeleo ya taifa.

Swaum amesema wanawake wakidharishwa katika mitandao ya kijamii inawafanya kuwa woga pamoja na kupata wakati mugumu katika familia zao.

Aidha amesema kuwa watu wanaotengeneza taarifa mbaya za wanawake kupitia mitandao ya kijamii wachukuliwe hatua ili hali hiyo isiweze kujirudia.

Aidha Swaum amesema kuwa hawawezi kumtaja mwanamke ambaye amesdhalilishwa na katika mitandao kwani kufanya hivyo ni kuendeleza udhalilishaji huo.
 Mjumbe wa WCP- Ulingo, Swaum Rashidi akizungumzia juu mitandao ya jamii inavyotakiwa kutumika katika maendeleo na sio kuchafua watu kulia ni anawakilisha  Walemavu WCP –Ulingo Agness Mgaya , kushoto ni  Mjumbe wa Sekretarieti wanawake wanasiasa WCP-Ulingo, Angelina Mtahiwa.
 Mjumbe wa Sekretarieti wanawake wanasiasa WCP-Ulingo, Angelina Mtahiwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya udhalilishaji wa wanawake baadhi ya mitando ya jamii si Michuzi Media, kulia ni  Mjumbe  Swaum Rashidi, kushoto  ni Mjumbe Diminatha Rwechungura.
Mjumbe wa Sekretarieti wanawake wanasiasa WCP-Ulingo, Angelina Mtahiwa (katikati )akionesha a mfano wa kutomtaja jina mwanamke jina aliyedhalilishwa katika mitandao ya kijamii kama vyombo vyaha habari vinavyoficha picha za wahusika katika matukio ya udhalilishaji leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad