HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 26 October 2017

TUPO TAYARI KUWAVAA AZAM KESHO AZAM COMPLEX- MBEYA CITY

KIKOSI cha timu ya Mbeya City kesho kinashuka dimbani kuvaana na timu ya Azam katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kwa ajili ya mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

Kuelekea mchezo huo,Meneja wa Mbeya City , Geoffrey Katepa amesema  kwamba wapo hapa tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazoezi yao Uwanja wa Uhuru na wakiwa wameweka kambi katika hostel za wokovu maeneo ya kurasini.

“Leo tumefanya mazoezi yetu ya mwisho hapa Uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo wetu wa kesho dhidi ya wenyeji wetu, Azam, dhamira kuu ikiwa ni kutopoteza tena mechi,”amesema.

Katepa amesema anafahamu mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu Azam watakuwa wanacheza nyumbani kwao, lakini watapigana kiume kuhakikisha wanawazima hapo hapo Azam Complex.

“Niseme tu kwamba tunawaheshimu wapinzani wetu, ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri na walimu wazuri. Lakini hata sisi tuna wachezaji wazuri na walimu wazuri na pia ni timu nzuri na ndio maana tupo kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu,”.

Amesema katika  mchezo huo anaamini utakuwa mgumu sana kwa pande zote na kwa sasaMbeya City inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi saba, ikizidiwa pointi moja na Singida United iliyo nafasi ya tano na inazidiwa pointi mbili na Azam FC iliyo nafasi ya nne.

Simba, Yanga na Mtibwa Sugar zote zinafungana kileleni mwa Ligi Kuu kwa kila timu kuwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi sana pia.

Mechi nyingine za Ligi Kuu zinatarajiwa kuchezwa Jumamosi, mabingwa watetezi, Yanga watamenyana na Simba, Uwanja wa Uhuru, Maji Maji wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mtibwa Sugar wataikaribisha Singida United Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro, Lipuli watakuwa wenyeji wa Mbao FC Uwanja wa Samora mjini Iringa na Kagera Sugar wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad