HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 5 October 2017

TCAA KUTUMIA ZAIDI YA SH. BILIONI 70 KWA AJILI YA MIUNDOMBINU YA MITAMBO


 Kaimu Mkurugenzi Huduma za Usafiri wa Anga wa TCAA,John Chambo akizungumza juu ya ununuzi wa mitambo mbalimbali ya kisasa watayofunga kwa ajili ya uongozaji ndege , jijini Dar es Salaam.
kulia ni Meneja wa Usafiri wa Anga uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere wa TCAA, Mwanajumaa Kombo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kozi mbalimbali kwa wanafunzi wa Wizara ya Ulinzi ya Uganda waliokuja kupata mafunzo katika chuo  cha mafunzo cha usafiri wa anga jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga , Dk. Daniel Kerenge akitoa historia ya chuo hicho katika utaoaji mafunzo mbalimbali ya usafiri wa anga jijini Dar es Salaam. 
Sehemu mitambo ya kupata taarifa za ndege zinazoingia nchini na zile zinazotumia anga ya Tanzania.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga (TCAA) kutumia zaidi ya sh.bilioni 70 kwa ajili ya miundombinu ya mitambo ya  kisasa itakayowezesha utekelazaji wa watumiaji wa usafiri anga kutumia miundombinu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kutembelea miundombinu mbalimbali katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ndege wa TCAA, John Chombo amesema miundombinu ya mitambo hiyo ni kwa ajili kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na teknolojia iliyopo kwa sasa katika usafri wa wa anga.

Amesema mitambo hiyo ikifungwa kazi itarahisha kwenda kisasa katika usalama wa ndege katika viwanja ndege kwa zile zinazoingia na kutoka katika anga ya nchini.

Chombo amesema miundombinu ya  mitambo mbalimbali  ya kuongozea ndege iliyopo bado inahimiri katika uongozaji wa ndege kinachofanya kununua ni kutokana na teknolojia iliyopo sasa ikiwa ni pamoja na uimarishaji huduma za usafiri wa anga.

Aidha amesema mitambo katika usafiri wa anga ni miaka 10 hivyo kila baada miaka hiyo inahitaji kubadilisha ili kwenda na mazingira yaliyopo pamoja na teknolojia iliyopo sasa inabadilika wakati kwa kuzingatia ni usalama wa ndege zinazoingia na kutoka.

Wakati huo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amefungua mafunzo kwa wanafunzi 24 wa Wizara ya Ulinzi ya Ulinzi ya Uganda katika kituo cha mafunzo cha usafiri wa anga cha TCAA.
Amesema nchi ya Uganda imekuwa ikileta watu wake katika kupata mafunzo mbalimbali ya usafiri wa anga kituo hicho kwani hivi karibuni walihitimu wanafunzi 17 katika kituo hicho wa mamlaka ya usafiri wa anga wa Uganda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad