HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 5 October 2017

DCB YAHAMASISHA WATEJA KUTUMIA HUDUMA DCB PESA POPOTE.

Moja ya wateja wa mda mrefu wa benki ya DCB Mama Fatma Simba akielezea namna benki hiyo ilivyweza kumsaidia katika shughuli zake za ujasiriamali mpaka alipofikia sasa na kuwataka wanawake waache tamaa pindi wanapochukua mikopo na kusifia pia huduma za DCB Pesa katika urahisishaji wa huduma za kipeki kupitia simu ya mkononi.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya DCB imesherehea wiki ya huduma kwa wateja kwa kufurahi pamoja na wateja wa benki hiyo huku wakiendelea kuwahamisha kutumia huduma ya DCB Pesa popote nchini.

Katika maadhimisho ya wiki kwa huduma kwa wateja, Afisa Mikopo wa DCB tawi la Magomeni Miriam Migetto amesema kuwa wanayofuraha ya kujumuika pamoja na wateja wa benki hiyo kusherehekea siku hii muhimu kwao pia na kuwasisitiza kuendelea kutumia huduma za kibenki.

Miriam amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kuboresha huduma za kibenki ikiwemo kutumia huduma ya DCB Pesa na DCB Jirani ikiwa ni katika kurahisisha huduma za kipesa kwa wateja wa DCB.

Afisa Mikopo wa DCB tawi la Magomeni Miriam Migetto akizungumza na wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ma kuwataka kuendelea kutumia huduma za kibenki kwa njia ya simu pamoja na kuendelea kuchukua mikopo ya riba nafuu.


Wafanyakazi wa tawi la benki ya DCB Magomeni wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo waliohudhuria kusherehekea maadhimisho ya wiki huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam leo.

Moja ya wateja wa muda mrefu wa benki hiyo, Mama Fatma  Simba amesema kuwa ameanza kutumia benki hiyo tangu mwaka 2005 na amekuwa akipata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi bila usumbufu na hata pia ameweza kupata mkopo wa bei nafuu na riba nafuu.

"Nimekuwa natumia DCB benki kwa zaidi ya miaka 12 na imeweza kunipatia mahitaji yangu kwa wakati ikiwemo mkopo wa bei nafuu na riba nafuu na hata katika utoaji wa huduma za kibenki kupitia DCB Pesa wameweza kutupunguzia wateja wao kwenda benki mara kwa mara, " amesema mama Fatma.

DCB benki wamesherehea wiki ya huduma kwa wateja katika matawi tofauti na kufurahi pamoja na wateja wao na kuahidi kuzidi kuboresha na  kuwapatia huduma wanazostahili na wakati sahihi.

Baadhi wa wafanyakazi wa Benki ya DCB Tawi la Mabibo External wakiwa katika picha ya pamoja  katika kuazimisha wiki ya huduma kwa wateja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad