HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 3 October 2017

STARTIMES WASHEREKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUZINDUA CHANELI MPYA KWA WATEJA WAKE


KATIKA kusherekea wiki ya huduma kwa wateja kampuni inayotoa huduma za ving'amuzi Tanzania Wamezindua chaneli mpya kwa wateja wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es aSalaam leo, Mkurugenzi wa uendeshaji wa Startimes, Carter Luoh amesema kuwa kampuni hiyo wameongeza chaneli mpya katika king'amuzi ambapo wanajisogeza karibu na wateja wake.

Pia amesema kuwa Startimes inafuraha kubwa kutoa huduma za kidijitali kwa mikoa 17 kwa kutoa huduma za ving'amuzi ambayo imewafikia wateja wa mikoa zaidi ya 17 hapa nchini kwa kuwafikia wateja kwa kufungua zaidi ya mawakala 300.

Kwaupande wake Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa Ngowi amesema kuwa katika wiki hii muhimu ya huduma kwa wateja wamezindua chaneli nyingine mpya kwenye king'amuzi cha startimes pamoja na pamoja na chaneli zitakazokuwa kimetafsiliwa kwa kiswahili pamoja na movi za kihindi.


 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua chaneli mpya ya kwenye king'amuzi cha Startimes katika wiki ya huduma kwa wateja.

 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh (katkati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Kampuni ya Startimes kuzindua chaneli mpya katika king'amuzi cha Startimes wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa wateja na kujiweka karibu zaidi na wateja wake. Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo na Kushoto ni Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa  ngowi.
 Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa  ngowi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua chaneli mpya ya king'amuzi cha Satrtimes katika kusherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba ikiwa ni kujiweka karibu zaidi na wateja wake. Amesema kuwa sherehe hizi zinaambatana na uongezwaji wa chaneli mpya kama vile ST Bollywood Afrika, ST Bollywood na FOX life. katikati ni Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh (katkati) na Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo.
 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akikata keki kwa pamoja na wateja wa king'amuzi cha Startimes kwaajili ya kusherekea wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akiwalisha keki wateja jijiji Dar es Salaam leo mara baada ya kufungua chaneli mpya katika king'amuzi cha startimes katika wiki ya huduma kwa wateja.

 Meneja wa mitambo wa Startimes, Yusuph Baracha akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuwatembeza katika chumba cha kurushia matangazo na vipindi mbalimbali vya king'amuzi cha startimes.
 Meneja wa mitambo wa Startimes, Yusuph Baracha akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuwatembeza katika chumba cha kurushia matangazo na vipindi mbalimbali vya king'amuzi cha startimes.
  Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa  ngowi akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.
Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo akizungumza na wateja wa startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad