HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 23, 2017

STAMICO SASA KULETA MAPINDUZI KWA WACHIMBAJI WADOGO

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico) limepata mtambo wa uchorongaji kwa kutumia upepo (Air Rotary Drill Rig) wenye thamani dola za Kimarekani milioni 1.3 utakaotumika kupata taarifa za kijiolojia na mashapo kwa wachimbaji wadogo .
Kunufaika kwa wachimbaji wadogo kunatokana na stamico kupata mtambo wa kisasa wa uchorongaji miamba.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico, Elexender Muganda amesema kuwa mtambo umetengenezwa nchini Canada ambapo  mtambo huo utasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa za kijiolojia na mashapo katika maeneo yao kwa gharama nafuu.
Amesema mtambo huo umetolewa na serikali kupitia Wizara ya Madini chiini ya ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa usimamizi endelevu wa rasilimali ya madini Tanzania (SMMRP).
Muganda amesema huo una uwezo wa kuchoronga miamba kwa kutumia upepo na kwa haraka zaidi kati ya kina mita 30 hadi 200 na kwa gharama ambazo mchimbaji mdogo anamudu na kuachana uchimbaji wa kubahatisha pamoja kuwezesha kupata mikopo katika taasisi za fedha.
Aidha amesema kuwa wachimbaji wadogo wanaohitaji huduma za uchorongaji kwa kutumia upepo wafike katika ofisi za Stamico ili kupata taarifa zaidi.
 Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico, Elexender Muganda akizungumza na waandishi habari juu shirika la Taifa la Madini (Stamico) kupata mtambo wa kisasa wa uchorongaji kwa kutumia upepo , jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Stamico, Alex Rutagwelela  akitoa ufafanuzi juu ya mtambo wa kisasa wa uchorongaji miamba jijini Dar es Salaam, kushoto ni Meneja Masoko na Uhusiano, Koleta Njelekela.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji, Alex Rutagwelela akiangalia mtambo wa uchorongaji wa miamba Bandarini, jijini Dar es Salaam.
 Muonekano wa mtambo  wa uchorongaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad