HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 26 October 2017

SPROXIL TANZANIA YAZINDUA TAALUMA YA KUGUNDUA BIDHAA BATILI

 Mkurugenzi mkuu wa Sproxil Africa Chinedum Chijioke akizungumza wakati wa uzinduzi wa teknolojia ya simu za mkononi kwa ajili ya kudhibiti bidhaa bandia na kumlinda mteja nchini Tanzania ikiwa na lengo la kutokomeza na kudhibiti wauzaji feki wa bidhaa mbalimbali zinazoingia sokoni.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KATIKA kudhibiti uuzwaji wa bidhaa bandia nchini, kampuni ya Sproxil Tanzania imezindua teknolojia ya simu za mkononi kwa ajili ya kudhibiti bidhaa bandia na kumlinda mteja nchini Tanzania.

Sproxil Tanzania imewezeshwa na mfuko wa maendeleo ya ubunifu wa bidhaa za binadamu duniani Human Development Innovation Fund (HDIF) imeweza kuwasilisha rasmi ubunifu bora wa namna ya kudhibiti bidhaa bandia kwa makampuni,taasisi za udhibiti na serikali.

Akizungumza wakati wa majadiliano ya wazi kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi mkuu wa Sproxil Africa Chinedum Chijioke amesema bidhaa bandia, batili, haramu na zilizochini ya kiwango ni hatari kwa afya za watumiaji wasio na hatia, upotoshaji wa bidhaa na pia zinateteresha ubora wa mwelekeo wa kiuchumi.

Chijioke amesema, uwepo wa bidhaa hizo na zisizo na sifa zinaathiri vibaya watumiaji na kuathiri sifa za wazalishaji ndio sababu hii imekuwa wajibu wa serikali za sekta binafsi kuwawezesha watanzania kutumia njia bora za udhibiti zinazoratibiwa na kampuni yao.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini Godfrey Simbeye amesifia teknolojia hiyo na kusema ni nzuri na itasaidia sana katika kudhibiti watengenezaji wa bidhaa bandia kuweza kuingiza bidhaa zao sokoni na kupelekea kwa watumiaji na pia teknolojia hii isiishie tu kwa bidhaa hizi bali ziende mpaka kwenye pembejeo za kilimo ikiwemo Mbolea na dawa za mazao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini Godfrey Simbeye akielezea namna teknolojia hiyo inavyoweza kuleta mapinduzi hususani kwa upande wa sekta binfasi kwani itasaidia kudhibiti uuzaji wa bidhaa bandia pamoja na kuwashauri kufika sekta ya kilimo hususani kwenye mbolea na dawa za kilimo.

"Teknolojia hii inatakiwa ifike mpaka kwa wakulima kwani wamekuwa wanapata shida sana kwani wanauziwa sana pembejeo ambazo ni bandia na kusababisha hasara, kwahiyo Proxil Tanzania wameleta njia sahihi sana na mategemeo yangu ni kuona wanakuja kutumia mfumo huo kwa wakulima,"amesema Simbeye.

Naye mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda Dr Samuel Nyatahe amesema wamiliki wa viwanda walikuwa wanapata tabu sana kupambana na bidhaa feki mtaani kwani wamekuwa wanauza vitu vyao kwa bei nafuu tofauti na wao wanaotengeneza bidhaa nzuri. Amesisitiza kuwa ni kosa la jinai na pia inafanya bidhaa kushuka thamani.

Licha ya kuzindua huduma ya udhibiti wa bidhaa halali ili kulinda makampuni ya Tanzania, pia wamesema watashirikiana na kutakuwa na zoezi la kuthibtisha ubora wa bidhaa chini ya usimamizi wa bodi ya viwango vya ubora wa bidhaa Tanzania (TBS) na ile ya bodi ya utawala wa bidhaa za chakula na udhibiti wa madawa (TFDA) na jopo la wawakilishi wa sheria na sekta binafsi.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda Dr Samuel Nyatahe akizungumza kwa upande wa sekta ya viwanda na kuelezea namna itakavyowasaidia katika kupambana na wauzaji wa bidhaa bandia ikiwemo kuwaondoa kabisa kwenye soko la ushindani.

Washiriki mbalimbali wakiwa wanafuatilia mjadala wa uzinduzi wa teknolojia ya huduma ya udhibiti wa bidhaa halali kwa ajili ya kulinda makampuni ya Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad