HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 14 October 2017

PRINCE AGHA KHAN AZINDUA STEMPU ZA POSTA ZENYE KUMBUKUMBU ZA TAASISI YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akiangalia picha za stempu zenye kumbukumbu ya Taasisi yake wakati alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, kabla ya kuzizindua jijini Dar es Salaam jana. Walioshika bango lenye picha za stempu hizo kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo. Anayeangalia kushoto ni Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akikabidhiwa bango lenye  picha za stempu zenye kumbukumbu ya Taasisi yake na kaimu postamasta  Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, wakati wa uzinduzi wa stempu hizo jijini jana. Anayeangalia kushoto ni Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Hussein Mwinyi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, mara baada ya kuzindua stempu hizo.
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan, akielezwa jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati akiangalia moja ya vikundi vya burudani vilivyotumbuiza katika uzinduzi huo. 
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (wa pili kulia), akimueleza jambo  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Hussein Mwinyi (kulia), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, baada  ya uzinduzi wa stempu hizo. 
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mara baada ya uzinduzi huo. 
Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, wakati wakizungumza jambo, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, baada ya uzinduzi wa stempu hizo.  
Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania (TPC), na kaimu Postamasta Mkuu Bw.Macrice Mbodo (kulia), akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa Shirika hilo, kwenye ofisi ya Posta uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere mara baada ya kumalizika uzinduzi huo.
Hizi ni baadhi ya stempu zenye kumbukumbu za taasisi ya Agha Khan zilizozinduliwa na kiongozi huyo jijini jana. 
Hii ni moja ya stempu yenye kumbukumbu ya taasisi ya Agha Khan zilizozinduliwa na kiongozi huyo jijini jana.

Hizi pia ni baadhi ya stempu zenye kumbukumbu za huduma mbalimbali za kijamii zinazofadhiliwa na taasisi ya Agha Khan nchini, zilizozinduliwa na kiongozi huyo jijini jana.

TAREHE 12 Oktoba, Mkuu wa Taasisi ya Agha Khan Foundation, Mtukufu Karim al-Hussayni  Agha Khan ambaye pia ni kiongozi Mkuu wa Jumuia ya Ismailia duniani na mtu anayeheshimika sana hasa kwa jamii ya Kihindi, alizuru nchini Tanzania na kufanya shughuli mbali mbali za Kitaifa na kibinafsi nchini.

Pamoja na kuwa na manufaa makubwa kwa nchi pia ziara hiyo ilikuwa muhimu sana kwa Shirika la Posta Tanzania.

Mbali na kutembelea miradi mbali mbali inayofadhiliwa na taasisi yake, alipata fursa ya kuzindua stampu zilizochapishwa na Shirika la Posta zinazoelezea au kuonyesha kumbukumbu muhimu za taasisi ya Agha Khan.

Uzinduzi wa stampu hizo ulifanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa ndege wa mwl.nyerere akiwa njiani kurudi ,baada ya ziara yake hapa nchini kukamilika.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi kwa niaba ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Joseph Pombe Magufuli ndiye aliyemkabidhi stampu hizo kutoka kwa Kaimu Postamasta Mkuu bw.Macrice Mbodo.

Stampu hizo, zenye kumbukumbu maalum za Agha Khan ni pamoja na jengo la dispensary ya zamani iliyojengwa na taasisi ya Agha Khan mjini Unguja pamoja na za picha za shughuli mbalimbali za kijamii zilizofadhiliwa na taasisi hiyo.

Uchapishaji wa stampu hizo, ulidhaminiwa na taasisi hiyo, kwa gharama ya shilingi milion 52, zikiwa ni stempu maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya Diamond Jubilee- miaka 60 ya tangu kusimikwa kwake kuwa Imamu Mkuu wa dhehebu la Shia Ismailia.

Mwaka 2007, taasisi ya Agha Khan waliweza pia kufadhili uchapishaji wa stampu maalum za kuadhimisha Golden Jubilee (1957-2007), kwa kiasi cha dola 10,573.24 .Stampu hizo zilikuwa na dhamani ya shilingi 267,059,000/=

Stampu hizo zitaweza kutumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida (postage) na zaidi kwa wakusanya stampu (stamps collectors), ambao mbali na kuweza kuzipata kupita kaunta za Posta na mawakala wa stampu, pia kwa sasa wanaweza kuzipata kupitia duka maalum (online) ambalo limeanzishwa na shirika la Posta.

Mteja yeyote akiwa popote Duniani anaweza kununua kupitia Web site ya Posta, ambapo ataingia kwenye kipengele cha e-busness na bonyeza e-service, kisha e-shop na atapata aina mbalimbali za stampu na maelekezo ya namna ya kununua. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad