HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 13 October 2017

MWANDAAJI MISS MBEYA AFUNGIWA RASMI KUENDESHA MATUKIO YA SANAA HAPA NCHINI

Na Agness Francis, Blogu ya jamii.
Baraza la Sanaa Taifa(BASATA) limemfungia rasmi mmiliki wa Click Media Entertainment, Edward Majura kujihusisha  kuendesha  matukio  yeyote ya sanaa hasa la utendaji wa mashindano ya urembo  hapa nchini kwa muda usiojulikana.
 Akizungumza hayo katibu mtendaji (BASATA) Godfrey Mngereza katika ofisi za (BASATA) jijini Dar es Salaam amesema kuwa Edward Majura ambaye ni mtendaji wa mashindano ya urembo miss Mbeya amekiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa  mashindano hayo hapa nchini .
Vilevile katibu Mngereza amewataka wadau na waandaaji wote wa matukio ya sanaa kuhakikisha wanafuata taratibu zote zilizowekwa  ikiwa ni pamoja na kupata vibali  na kufanya kazi kwa karibu na ofisi za utamaduni katika ngazi za wilaya na kimkoa pindi wanapohitaji kufanya tukio lolote la sanaa na hapa nchini.
Aidha Katibu mtendaji huyo ametanabaisha kuwa muandaaji yoyote atakae tumia wakala walioko nchini katika tukio lake la sanaa atawajibika kuhakikisha wako chini yake na wanafata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa tukio husika, ambapo kinyume na makubaliano hayo ( BASATA) haitasita kumchukulia hatua yoyote ya kisheria.
Hata hivyo Mngereza ametoa tamko kuwa  wadau wote nchini watakaoendesha  matukio yoyote ya sanaa ikiwemo  mashindano ya urembo wanatakiwa  kuwasilisha zawadi zao sehemu husika ambayo ni  (BASATA) katika ofisi za utamaduni siku 14 kabla ya kilele cha mashindano hayo.

Katibu mtendaji (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa sanaa nchini kuhusu kufata kanuni na taratibu za kufanya matukio ya sanaa hasa na mashindano ya urembo katika ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad