HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 18 October 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA IRELAND

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi katika Idara ya Mambo ya Nje na Biashara mwenye Jukumu Maalum kwa ajli ya Diaspora na Maendeleo ya Kimataifa wa Ireland Mhe. Ciaran Cannon aliyeambatana na Balozi wa Ireland nchini Tanzania.
Katika mazungumzo yao walitilia mkazo katika masuala ya Biashara na uwekezaji hasa ikizingatiwa kwamba nchi zote mbili mazingira yake yanaruhusu .
Makamu wa Rais alimuambia Waziri huyo Tanzania ni nchi nzuri na rafiki kwa kuwekeza hivyo wanakaribishwa kuwekeza hasa katika viwanda na teknolojia, Waziri huyo alieleza kuridhishwa kwake  na jitihada za Tanzania katika kusimamia uchumi wake kwa ujumla.
Mheshimiwa Makamu wa Rais alielezea vifo vya wakina mama kabla na wakati wa kujifungua na watoto wachanga na kuiomba Serikali ya Ireland kupitia Waziri huyo kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo hilo, ambapo waziri huyo alioneshwa kuguswa sana hasa pale Makamu wa Rais alipoelezea uzoefu wake mwenyewe aliowahi kukutana nao wakati anajifungua mtoto wake wa tatu.
Makamu wa Rais na Waziri huyo kutoka Ireland kwa pamoja walikubaliana katika suala zima la kuboresha elimu, mafunzo  na kubadilishana ujuzi hasa katika masuala ya Afya, Teknolojia na Anga.
Mwisho Makamu wa Rais alisema Ushirikiano wa nchi mbili hizi ni wakudumu na kuiomba Serikali ya Ireland kuendelea kushirikiana na kusaidia Tanzania.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nchi katika Idara ya Mambo ya Nje na Biashara mwenye Jukumu Maalum kwa ajili ya Diaspora na Maendeleo Kimataifa wa Ireland Mhe. Ciaran Cannon aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam akiongozana na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada la Irish Ndugu Ruairi De Burca's. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi katika Idara ya Mambo ya Nje na Biashara mwenye Jukumu Maalum kwa ajili ya Diaspora na Maendeleo Kimataifa wa Ireland Mhe. Ciaran Cannon mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad