HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 3 October 2017

FILAMU YA BEI KALI KUZINDULIWA RASMI KESHO MLIMANI CITY

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

FILAMU ya Bei Kali inatarajiwa kuzinduliwa kesho katika ukumbi wa Mlimani City Golden Premier huku wasanii wakijinasibu kuwa ni moja kati ya filamu bora ndani ya soko la filamu.

Filamu hiyo inayojulikana kwa jina la 'Bei Kali' itazunduliwa rasmi kesho kuanzia saa moja usiku ikiwa mbashara kupitia kituo cha televisheni cha Azam Tv kwenye chaneli ya Sinema zetu na kuanza kuingia mtaani.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Daud Michael 'Duma' amesema kuwa filamu hiyo iliyofanywa chini ya Kwetu Studio imeweza kuchukua waigizaji wakubwa akiwemo Irene Uwoya, Hemed Suleiman, Patcho Mwamba na Kaptu Rado.

Duma amesema kuwa filamu hiyo inayoelezea maisha ya kawaida yenye mahusiano ndani yake yakimuhisha mwanadada aliyetoroshwa na mwanaume mwingine na kuletwa mjini lakini alipofika akajiingiza katika mahusiano mengine tofauti na baadae mumewe akaja kumtafuta mjini.

Ameeleza kuwa, filamu hiyo imejaa uhalisia zaidi na ana imani wapenzi wa filamu za kitanzania wataoendezewa nayo kwani imeweza kugusa maisha hali ya kitanzania hasa katika mahusiano na ndoa.

Filamu hiyo, imesimamiwa na Kaptu Rado sambamba na Rashidi Mrutu ambapo Duma amesema itakuja kuwakamata mtaani kwa ubora mzuri na hata waigizaji wake wameweza kutendea haki sehemu walizopatiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad