HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 10, 2017

BAADHI YA WANAFUNZI WAKIKE WANUFAIKA NA ELIMU TOKA VODACOM TANZANIA YA KUSHIKA NYADHIFA MBALIMBALI KATIKA JAMII KUELEKEA SIKU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE KESHO.

IKIWA ni kuelekea siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho,Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, Imeanza kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa kutoa elimu ya uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho kwa baadhi ya wanafuzi wakike wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo mbezi Beach jijini Dar as Salaam.

"Akiongelea kuhusiana na mafunzo waliyokuwa wanayatoa kwa wanafunzi hao,Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Jacquiline Materu alisema wamefurahia sana kupata frusa ya kuwafundisha wasichana hao na kuwapa motisha kwamba hakuna mipaka ya kufikia malengo yao ya hapo baadaye bali ni juhudi zao wenyewe kamwe wasije kukata tamaa kwani wanaweza"Alisema Materu.

Mkuu huyo alifafanua zaidi kwamba pamoja na kuwawezesha wanawake na kukuza usawa wa kijinsia ni muhimu kuharakisha maendeleo endelevu. Kumaliza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana ili haki za msingi za kibinadamu ziweze kufanyiwa kazi kwani kuna athari nyingi kwa maeneo ya Taifa letu. Alisema.

"Bado hakuna usawa katika upatikanaji wa ajira na ulipwaji wa mishahara ulimwenguni na bado kuna mapungufu makubwa kati ya wanaume na wanawake katika soko la ajira"
Mkuu wa kitengo cha ripoti na taarifa M-Pesa,Nelusigwe Mwangota(kushoto)akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam,kuhusiana na uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia ,Wanafunzi hao walitembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania PLC moroko jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Domician Mkama kuhusiana na uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia ,Wanafunzi hao walitembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo moroko jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam waliotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania PLC yaliyopo moroko jijini Dar es Salaam,wakipokea zawadi toka kwa Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Harriet Rwakatare baada ya kuwaelimisha juu ya uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia.
Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Harriet Rwakatare akipiga selfie na baadhi ya wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania PLC yaliyopo moroko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mafunzo ya uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii waliyopatiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi baadhi ya wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam wakati wanafunzi hao walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo moroko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza njinsi ya uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii elimu hiyo ilitolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia.

Mkuu wa kitengo cha cha maduka ya rejareja ya Vodacom Tanzania PLC, Brigita Stephen(kushoto)akiongea na baadhi ya wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam kuhusiana na uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia ,Wanafunzi hao walitembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo moroko jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad