HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 24, 2017

24 WAITWA STARS KWA AJILI YA KUIVAA BENINI NOVEMBA 11

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji  24 ambao watacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Benini mapema mwezi ujao.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji  24 ambao watacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa mapema mwezi ujao.

Baada ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars sasa itatoka mwezi ujao kwenda Benin kucheza na wenyeji Novemba 11, mwaka huu.


Mayanga ameita kikosi cha wachezaji 24 ambacho kitaingia kambini Novemba 5 mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo na amewarejesha kikosini kiungo Farid Mussa na mshambuliaji, Elias Maguri kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki . 

Katika kikosi hicho amewaorodhesha Maguri aliyekuwa anacheza Oman na Farid Mussa anayecheza Tenerife B ya Hispania, ambao wote hakuwaita kwenye mchezo uliopita dhidi ya Malawi, uliomalizika kwa sare ya 1-1 Oktoba 7, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 

Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo kinaundwa na makipaAishi Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili, mabeki Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afruka Kusini), Gardiel Michael (Yanga), Kevin Yondan (Yanga), Nurdin Chona (Prisons), Erasto Nyoni (Simba) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba), Raphael Daudi (Yanga), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Ibrahim Hajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid Mussa (Tenerife/Hispania) na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya) na washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Azam FC), Elias Maguri (Huru) na Yohanna Nkomola (Huru). 






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad