HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 11 September 2017

ZIMAMOTO MBEYA WAANZISHA KLABU ZA ZIMAMOTO MASHULENI

 Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa  Mbeya  limeanza rasmi kufungua klabu za zimamoto  mashuleni  ikishirikisha Skauti toka shule zote zilizopo Mbeya mjini kuanzia tarehe 8/ 9/2017 hadi 10/9/2017 huku zoezi   likitarajiwa kuendelea katika wilaya nyingine zilizopo ndani ya halmashauri ya jiji la Mbeya.                                     
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh.William Ntinika akizungumza wakai wa ufunguzi wa klabu za zima moto ya halmashauri ya  Mbeya Mjini.

 Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh.William Ntinika aliambatana na  mkuu wa mafunzo wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya mkaguzi msaidizi Hashim Mwembe  na kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya Sadock Ntole katika uzinduzi wa klabu za Zimamoto katika halmashauri ya  Mbeya mjini. 
Mkuu wa wilaya ya mbeya mjini Mh.William Ntinika akipatiwa elimu ya matumizi sahihi ya vifaa vya kuzimia moto na maokozi ndani ya uwanja wa mwinyi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad