HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 11, 2017

USHIRIKIANO WA NMB NA VIGUTA KUWANUFAISHA ZAIDI YA WANACHAMA 100

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda wakisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Wengine wanaoshuhudia ni maofisa kutoka benki ya NMB na Viguta.

Zaidi ya wanachama 100 watanufaika na Ushirikiano baina ya Benki ya NMB na Umoja wa Vicoba Tanzania (VIGUTA), baada ya kutiliana saini ya mkataba wa ushirikiano.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini mkataba huo wa ushirikiano jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker alisema leo ni siku ya kipee kwa benki hiyo kwa kusaini mkabata wa ushirikiano na Viguta ambao utafungua ukurasa mpya katika sekta ya kifedha nchini.

Alisema benki hiyo siku zote imekuwa karibu na wananchi katika utoaji wa huduma zake na katika ushirikiano huo itatoa mafunzo ya utunzaji wa fedha kwa wateja wao.

Alisema huduma watakayoweza kunufaika nayo wanachama ni ile ya akaunti ya pamoja kupitia vikundi ambapo wanachama wao wataweza kukopa mikopo yenye riba nafuu na kuweza kujua mambo mbalimbali kama kujua salio kwa kutumia simu zao za mkononi.

Alisema benki hiyo imejipanga vizuri kutoa huduma kwa wateja wao pamoja na kutoa elimu kwa kila mtu na ushirikiano huo utakuwa ni endelevu.

Alisema wanaounda akaunti ya pamoja ni makundi ya watu kutoka katika familia, makundi ya wanawake, marafiki na makundi ya whatsApp.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda alisema umoja huo una wanachama milioni 7 huku ukiwa na vikundi 92,000 ambao wananufaika na benki hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda wakibadilishana hati baada ya kutiliana saini. Kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na Wakati wa NMB, Abdulmajid NsekelaAbdulmajid Nsekela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda.

Taswira meza kuu.

Wanachama wa Viguta wakiwa kwenye mkutano huo.

Viongozi mbalimbali wa Viguta.

Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na Wakati wa NMB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Viguta, Eva Mbone.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda, akizungumza.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo, Wateja Rejareja, Omari Mtiga akizungumza.
Mada ikitolewa.

Majadiliano yakifanyika.

mkutano ukiendelea.

Wafanyakazi wa NMB wakijadiliana.
Meneja Mwandamizi wa Huduma na Amana wa NMB, Stephen Adili akijibu maswali.

Wanakikundi wakiwa kwenye mkutano huo.

Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad