HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 20 September 2017

WATUMISHI WANNE NA MZABUNI MMOJA WA IGUNGA WASWEKWA MAHABUSU KWA TUHUMA ZA UDANGANYIFU KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA TIBA

Na Tiganya Vincent
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa watumishi wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga na Mzabuni Muhoro Traders kwa tuhuma za udanganyigu wa ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 23.2.
Agizo hilo limetolewa leo mjini Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Amesema kuwa kwa nyakati tofauti za kuanzia Januari  na Machi mwaka huu watumishi walikula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu jumla ya shilingi milioni 23,202.500.00 mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Mwanri anaongeza kuwa watumishi hao waliagiza vifaa hivyo kutoka kwa Mzabuni Muhoro Traders wa Igunga vifaa , lakini havikuwahi kupokelewa na Halmashauri ya Igunga lakini kwenye vitabu vya Afisa Ugavi na yule wa Bohari walikiri kupokea katika vitabu vyao.
“Naagiza watumishi hao wanne wasimamishwe kazi na wakamatwe wao na Mzabuni Muhoro Traders kisha wawekwe ndani kwa ajili ya kufikishwa  Mahakamani ili wajibu tuhuma zinazowakabili” anasema Mkuu huyo wa Mkoa.
Anasema kuwa katika hati namba ya malipo namba 2071-1457 watuhumiwa walichukua shilingi 9,250,000/-, hati namba 2017-1457 walijipatia shilingi 6,850,000/- na hati ya malipo namba 2017-1453 shilingi 7,102,500/- na kusababishia Halmashauri hasara hiyo.
Mwanri amewataja walikamatwa ni pamoja na aliyewahi kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga Gidfrey Mgongo, Afisa Ugavi Mohamed Mtao, aliyekuwa Mhasibu wa Idara ya Afya sasa yuko TARURA Richard Byelembo, Boharia wa Idara ya Afya Jones Lotto.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza pia Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga wa sasa Dkt. Bonaventura Kalumete ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri amewaagiza kushughulikia tatizo la ukosefu wa dawa katika Zahanati kwa sababu tayari Halmashauri hiyo imepokea miliomi 550 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad