Tetemeko kubwa la ardhi limeikumba
Mexico na kuua watu karibu 250 na kuangusha makumi ya majengo katika
mji mkuu wa Mexico City.

Rais Enrique Peña Nieto amesema
zaidi ya watoto 20 wamekufa na 30 hawajulikani walipo baada ya jengo
la shule kuanguka.
Tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa
wa alama 7.1 limesababisha uharibifu mkubwa katika majimbo ya jirani
na Mexico City.
Waokoaji wakiendelea na shughuli ya uokoaji kwa kufukua vifusi vya majengo
No comments:
Post a Comment